METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, May 12, 2023

MBUNGE KASSIM AIOMBA SERIKALI KUPELEKA VIFAA TIBA NA WAUGUZI KATIKA JIMBO LA MSALALA


Na Saida Issa, Dodoma

MBUNGE wa Msalala Iddi Kassim ameiomba Serikali kuweza kupatiwa vifaa Tiba katika zahanati 24 na watumishi kwani katika Jimbo hilo kuna upungufu wa watumishi wa Afya.

Hayo ameyaeleza Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akichangia katika bajeti ya Wizara ya afya Kwa mwaka wa fedha 2023/24 amesema kwamba kwa sasa wapo watumishi zaidi ya 264 tu na kunaupungufu wa watumishi zaidi ya 500.

" Nikuombe Mheshimiwa Waziri tusaidie tuweze kupata watumishi kwa sababu tumekamilisha maboma ya zahanati kwenye Kila Kijiji lakini changamoto iliyopo sasa hivi ni vifaa Tiba lakini na watumishi ambao wataenda kutusaidia kuziendesha zahanati hizo,

Mheshimiwa Naibu Waziri alifika na amezishuhudia zahanati hizo zipo kazishuhudia kwa macho yake na sasa wananchi wanaenda kufanya kazi ya Usafi kwenye  maeneo Yale wakisubiri vifaa Tiba lakini pia na watumishi,"amesema Mbunge huyo.

Aidha ameshukuru Dkt.Samia Kwa kushirikiana na wadau wa Barrik kwa kuweza kuwapatia Milioni 400 kwaajili ya kupunguza changamoto ya watumishi hivyo kuweza kujenga Chuo Cha afya ambacho hivi karibuni kinakwenda kukamilika.

"Nikuombe Mheshimiwa Waziri muweze kufika ma kukifungua Chuo hiki ili kiweze kuwasaidia wananchi kwani kitazalisha wauguzi ambao watakwenda kumaliza changamoto ya wauguzi,"amesema.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com