METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, May 13, 2023

MBUNGE GANDO AWATAKA WAUGUZI KUWA NA KAULI NZURI KWA WAGONJWA

Na Saida Issa, Dodoma

MBUNGE wa Gando Salim Mussa Omar amewataka wauguzi kuwa na Kauli nzuri katika maeneo yao ya kazi kwani imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wananchi hasa wanapo kwenda kupata matibabu.

Mbunge huyo ameyasema hayo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa tabia ya wauguzi kutowajali wagonjwa imekithiri hasa katika hospitali za Serikali.

"Mimi hii iliwahi nitokea tena katika hospital kubwa ya serikali nilienda kumsamilia mwananchi wangu wajimboni nilipofika Hospitali kumuuliza muuguzi alinijibu vibaya ikabidi nitafute muuguzi mwingine nimuulize na alipofahamu kuwa mie ni mbunge alitaka kuniomba radhi lakini mie nikawa nimeshajia kuwa hii ni tabia yao,"amesema.

Pia amesisitiza kuwa wauguzi waache kitizama mtu Kwa cheo kwani wao wapo kwaajili ya kuwatumikia watanzania na vyeo hivyo wanapewa na wananchi hivyo nivyema wakasimamia maadili ya kazi zao.

"Kiukweli hivi vyeo tunapewa na wananchi na wao walisema hawakutaki unabaki kuwa mtu wa kawaida sasa muhimu kuwaheshimu na kuwapa huduma zinazostahili sio kumuhudumia mtu kulingana na na cheo chake,"amesisitiza.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com