Na Saida Issa,Dodoma
MFUKO wa Mawasiliano kwa wote UCSAF katika kuendelea kuadhimisha siku ya wanawake imtoa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni nane laki tatu na hamsini kwaajili ya watoto wenye mahitaji mbalimbali wa kituo cha watoto cha Tumaini Foundation kilichopo kata ya ihumwa halmashauri ya jiji la dodoma.
Akizungumza
wakati wakuwasilisha vifaa hivyo Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote
UCSAF Yustina Mashiba aliesema Mfuko umeona vyema kuadhimisha siku ya wanawake
kwakuona watoto wenye mahitaji ili kuwapa moyo kwakuiona thamani yao katika
jamii.
Aidha Mashiba
alitoa wito kwa jamii hususani wazazi na walezi, na watu kutoka madhehebu
mbalimbali kuwa na utamaduni wakuwafundisha watoto wao kuwajali watu wenye
mahitaji kwani hakuna binadamu aliyezaliwa nakuchagua awe nani na hawajui
watoto wao watakuja kulelewa na nani pindi watakapokumbwa na changamoto
mbalimbali kama ajali au kifo.
"Sisi hapa
tulipo hakuna anayeijua kesho yake kuna mahali nilisoma pameandikwa mtoto wako
wa Leo ni yatima wa kesho hivyo natamani tuwe na desturi ya kuishi kwa
kusaidia,
Sababu hata sisi
hatujui watoto wetu nani atawasaidia hapo baadae hata hawa hawakujua kama
wataishia hapa,nashauri mtu akipata wazo la kutembelea kituo chochote aende na
watoto wake ili wajifunze hii inaanzia kwa watoto wakiwa wadogo hatawakikuwa
watakuwa na tamaduni ya kusaidia,"alisema.
Awali
akizungumza wakati wakupokea vifaa hivyo Tumaini Raymond Kivuyo Mkurugenzi
Mtendaji wa Tumaini Foundation alisema kituo hicho kina jumla ya watoto 350
ambao wanachangamo mbalimbali kama vile watoto wenye ulemavu, wanaoishi kwenye
mazingira magumu, na wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Aliongeza kuwa
Tumaini Foundation imekua ikihakikisha watoto wanaolelewa kituoni hapo
wanachukuliwa kutoka maeneo ambayo hayafikiki, waliofichwa na hawakua na
tumaini la maisha hivyo huwachukua nakuwapa ushauri ili wajione wenye thamani
katika jamii.
"Tunachukua
watoto kutoka katika maeneo tofauti tofauti hasa maeneo ambayo hayafikiki na
hawa watoto wanamatatizo mbalimbali lengo letu sisi ni kuwafanya watoto hawa
wawe na matumaini sababu wengine tayari wameshapoteza matumaini kwa kuondokewa
na Wazazi wao,"alisema.
Alisema watoto
wanapokuwa kituoni hapo hufundishwa mambo mbalimbali kama vile kujitegemea,
kuendeleza vipaji vyao sambamba nakuhakikisha wanashiriki shughuli zakiuchumi
wanapofikisha umri wa miaka 18.
Katika hatua
nyingine Tumaini alisema wamekua na program mbalimbali za kuhamasisha jamii
kuwa sehemu ya malezi kwa watoto hao ili kuwafanya watoto wapate upendo huku
akitoa wito kwa jamii, serikali na mashiririka mbalimbali kuwa sehemu
yakuhakikisha watoto hao wanafikia ndoto zao.
Akitoa neno la
shukrani kwa niaba ya watoto waliopo kituoni hapo Mtoto Suzana Zakayo alisema
anaushukuru Mfuko wa mawasiliano kwa wote kupitia wanawake ambao wameguswa
nakuona haja yakwenda kuwaona huku akiwaombea Mungu awabariki na kuzidisha
walipotoa kwa moyo wa upendo.
Vifaa
vilivyotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF ni pamoja na magodoro,
mashuka, Neti, Sabuni, maziwa, mchele, maharage, mafuta ya kupikia, sukari,
tambi, unga wa ngano, Sembe na vifaa vingine vyote jumla vikiwa na thamani ya
shilingi milioni nane laki tatu na hamsini.
Mfuko wa
mawasiliano kwa wote ulianzishwa chini ya Sheria ya Upatikanaji wa huduma ya
Mawasiliano kwa Wote; Sura 422 ambayo ilikubaliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mnamo Januari 2007. Ikiwa na jukumu la Kuhamasisha
ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za Mawasiliano
kwa Wote katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye Mawasiliano
hafifu.
0 comments:
Post a Comment