Tuesday, March 28, 2023

UCSAF YAREJESHA FURAHA KATIKA KITUO CHA TUMAINI KWA KUTOA VIFAA MBALIMBALI





Na Saida Issa,Dodoma

MFUKO wa Mawasiliano kwa wote UCSAF katika kuendelea kuadhimisha siku ya wanawake imtoa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni nane laki tatu na hamsini kwaajili ya watoto wenye mahitaji mbalimbali wa kituo cha watoto cha Tumaini Foundation kilichopo kata ya ihumwa halmashauri ya jiji la dodoma.

Akizungumza wakati wakuwasilisha vifaa hivyo Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF Yustina Mashiba aliesema Mfuko umeona vyema kuadhimisha siku ya wanawake kwakuona watoto wenye mahitaji ili kuwapa moyo kwakuiona thamani yao katika jamii.

Aidha Mashiba alitoa wito kwa jamii hususani wazazi na walezi, na watu kutoka madhehebu mbalimbali kuwa na utamaduni wakuwafundisha watoto wao kuwajali watu wenye mahitaji kwani hakuna binadamu aliyezaliwa nakuchagua awe nani na hawajui watoto wao watakuja kulelewa na nani pindi watakapokumbwa na changamoto mbalimbali kama ajali au kifo.

"Sisi hapa tulipo hakuna anayeijua kesho yake kuna mahali nilisoma pameandikwa mtoto wako wa Leo ni yatima wa kesho hivyo natamani tuwe na desturi ya kuishi kwa kusaidia,

Sababu hata sisi hatujui watoto wetu nani atawasaidia hapo baadae hata hawa hawakujua kama wataishia hapa,nashauri mtu akipata wazo la kutembelea kituo chochote aende na watoto wake ili wajifunze hii inaanzia kwa watoto wakiwa wadogo hatawakikuwa watakuwa na tamaduni ya kusaidia,"alisema.

Awali akizungumza wakati wakupokea vifaa hivyo Tumaini Raymond Kivuyo Mkurugenzi Mtendaji wa Tumaini Foundation alisema kituo hicho kina jumla ya watoto 350 ambao wanachangamo mbalimbali kama vile watoto wenye ulemavu, wanaoishi kwenye mazingira magumu, na wanaoishi na virusi vya ukimwi.

Aliongeza kuwa Tumaini Foundation imekua ikihakikisha watoto wanaolelewa kituoni hapo wanachukuliwa kutoka maeneo ambayo hayafikiki, waliofichwa na hawakua na tumaini la maisha hivyo huwachukua nakuwapa ushauri ili wajione wenye thamani katika jamii.

"Tunachukua watoto kutoka katika maeneo tofauti tofauti hasa maeneo ambayo hayafikiki na hawa watoto wanamatatizo mbalimbali lengo letu sisi ni kuwafanya watoto hawa wawe na matumaini sababu wengine tayari wameshapoteza matumaini kwa kuondokewa na Wazazi wao,"alisema.

 

Alisema watoto wanapokuwa kituoni hapo hufundishwa mambo mbalimbali kama vile kujitegemea, kuendeleza vipaji vyao sambamba nakuhakikisha wanashiriki shughuli zakiuchumi wanapofikisha umri wa miaka 18.

Katika hatua nyingine Tumaini alisema wamekua na program mbalimbali za kuhamasisha jamii kuwa sehemu ya malezi kwa watoto hao ili kuwafanya watoto wapate upendo huku akitoa wito kwa jamii, serikali na mashiririka mbalimbali kuwa sehemu yakuhakikisha watoto hao wanafikia ndoto zao.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya watoto waliopo kituoni hapo Mtoto Suzana Zakayo alisema anaushukuru Mfuko wa mawasiliano kwa wote kupitia wanawake ambao wameguswa nakuona haja yakwenda kuwaona huku akiwaombea Mungu awabariki na kuzidisha walipotoa kwa moyo wa upendo.

Vifaa vilivyotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF ni pamoja na magodoro, mashuka, Neti, Sabuni, maziwa, mchele, maharage, mafuta ya kupikia, sukari, tambi, unga wa ngano, Sembe na vifaa vingine vyote jumla vikiwa na thamani ya shilingi milioni nane laki tatu na hamsini.

Mfuko wa mawasiliano kwa wote ulianzishwa chini ya Sheria ya Upatikanaji wa huduma ya Mawasiliano kwa Wote; Sura 422 ambayo ilikubaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Januari 2007. Ikiwa na jukumu la Kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za Mawasiliano kwa Wote katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye Mawasiliano hafifu.

 

 

No comments:

Post a Comment