Na Hamis Hussein – Singida
MWENYEKITI wa
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida Martha Mlata amewataka wanachama na
wananchi wa Manyoni kutoa ushirikiano kwa serikali katika zoezi la kubaini watu
wanaohusika na mauaji ya watu.
Mlata amesema
hayo Jana Machi 15, 2023 wakati akizungumza na wanachama wa CCM Wilayani humo
ambapo amewataka wanachama wa CCM na wananchi wa Manyoni kwa ujumla kuwa
wa kweli kwa kutoa taarifa za ushaidi kwa serikali wakati wa kubaini watu
wanaohusika na mauaji yanayotishia amani Wilayani Humo.
"Tulimwita Mkuu wa mkoa na kazi
imeanza, ukija kuulizwa kama unajua jambo usikatae Sema ukweli kuisaidia serikali na kama unashindwa funga
safari kwa Mkuu wa Mkoa ukamwambie muitonye serikali, naomba mtulie na Waziri
wa Mambo ya Ndani alikuja kwahiyo haya mambo yanaendelea kufanyiwa kazi na
wakianza kukamatwa msiwape dhamana."
Alisema Mlata.
Aidha ameongeza kwa kuwataka wananchi hao kutumia chama cha Mapinduzi Kuwasilisha kero zao ili zitatuliwe kwa haraka
kwa kuwa chama hicho kipo kwaajili ya kuwahudumia watu hasa pale inapojitokeza
changamoto.
"Ukitaka changamoto zako zitatuliwe
kwa haraka leta kwenye Chama, kwahiyo kero zote tuzifikishe kwenye chama ili
chama kitapeleka serikalini tuna
Madiwani, Wabunge, Watendaji wa Vijiji na kata, Wenyeviti wa halmashauri, tuna
Wakurugenzi, Mkurugenzi akiitwa na Mwenyekiti wa Chama atatekeleza" Alisema Mlata.
Naye MNEC Mkoa
wa Singida Yohana Msita Amewahimiza wananchi wa Manyoni kuungana kuwa kitu
Kimoja katika kupambana na watu wanaotaka kuirudisha Manyoni nyuma ili
kuchochea Maendeleo katika nyanja Mbalimbali.
Msita alisema
kuna watu bado wanachochea watu kutengena na kugawanyika jambo ambali
alilikataa na kuwataka wananchi kuwa pamoja katika kuzikabili changamoto za
namna ile.
"Wanamanyoni Lazima tuunganie tuwe
kitu Kimoja asiwepo mtu wakutupasua,watukugawa huyo atatuchelewesha kwenye
maendeleo wapo baadhi ya watu hawatutakii mema wanatamani watuone tumegawanyika
tumepalanganyika ili yasiwepo maendeleo lakini sisi Watu wa Manyoni tunatakiwa
kupinga kwa nguvu Kubwaa, tumuone kuwa ni adui mkubwa mtu anayetugawa
anayetupalaganyisha ule umoja, upendo tuudumishe." Alisema Msita.
Awali Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Wilayani humo Jumanne Ismail alizitaja changamoto ambazo
zimekuwa kero kwa wananchi jambo ambalo linawapa wakati mgumu pindi wanapo
kutana nao.
Alizitaja
changamoto hizo kuwa in Pamoja na kukithiri kwa mauji ya watu ambapo chama
hicho kimeendelea kulaani, jambo jingine ni kukatika kwa Umeme hali
inayokwamisha shuguli nyingi za uzalishaji jambo alilolitaja kuwa changamoto hiyo inakipunguzia chama cha Mapinduzi kura kwa wanachama wake.
Aidha suala
lingine ambalo bado ni kitendawili ni kutokuwepo kwa usawa kwenye ugawaji wa
Mahindi ya ruzuku ya serikali ambapo baadhi ya kata hazijapata Mahindi mpaka
sasa akitolea mfano kata Rungwa iliyompakani mwa Singida na Mkoa wa Mbeya.
0 comments:
Post a Comment