METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 15, 2023

NAIBU WAZIRI MHANDISI KUNDO AMPONGEZA MSHINDI TUZO ZA WSIS


Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Kundo A. Mathew akimpongeza mshindi wa tuzo za WSIS kutoka taasisi ya Apps and Girls Tanzania Bi. Carolyne Ekyarisiima, katika kipengele cha ajira kwa njia ya mtandao kupitia mradi wao wa ujasiriamali kwa wasichana kupitia TEHAMA.

Tuzo hizo zimetolewa kwenye kongamano la Jumuiya ya Habari na Mawasiliano Ulimwenguni (WSIS), linalofanyika jijini Geneva , Uswizi kuanzia tarehe 13 hadi 17 Machi, 2023 kwa lengo madhubuti la kujadiliana na kuweka mikakati ya kuendelea kuboresha sekta ya habari na Mawasiliano kupitia TEHAMA.

Apps and Girls wamepeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuwa washindi pekee kwa nchi za Afrika Mashariki kwenye mashindano yaliyoandaliwa na WSIS Mwaka 2022-2023.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com