Pia, Prof Mkenda amesema ni kweli utandawazi hasa masuala ya simu yamewezesha taarifa ambazo zinawashawishi watoto kwenda kufanya mambo ambayo ni mabaya na kwamba suala la malezi ni jambo la mtambuka kwani linaanzia nyumbani mpaka shuleni.
Waziri Mkenda ameyasema hayo Januari 21, 2023 Jijini Dodoma katika kikao cha Wadau wa Elimu wa Shule binafisi ambacho pia kimehudhiriwa na viongozi wa Idara mbalimbali zilizopo chini ya Wizara hiyo na kuongeza kuwa kama kuna watu wanafanya kampeni na kuona suala hilo lipitie shuleni kwa watoto ni lazima Shule hizo ziwekewe ulinzi.
Prof. Mkenda amesema kuwa dunia nzima hasa nchi za Magharibi hakuna nchi inayoruhusu mambo ya ngono kwa watoto na kuwataka Wakuu wa shule binafsi kuangalia vitabu vyote vimeandikwa maudhui gani.
"Kama ni kweli kuna watu wanafanya kampeni na kuona hili suala lipitie shuleni kwa watoto wetu ina maana shule zetu lazima ziwe na ulinzi mkubwa sana," amesema Waziri Mkenda
Ameongeza kuwa kazi ya ulinzi kwa watoto ni jambo muhimu na kwamba hakuna kigugumizi katika kulisemea suala hilo.
Prof. Mkenda amebainisha kuwa shule zote za binafisi zina umuhimu mkubwa kwa serikali na kwamba wanathamini mchango wa shule hizo.
CREDIT, Ihojo Media
0 comments:
Post a Comment