Agizo hilo limetolewa na mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda wakati akiongea na Watendaji wa kata, vijiji, Maafisa Elimu kata, wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari. Januari 20 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba.
Akizungumzia suala la Uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza,Dc Mwenda amewataka waandikishaji wilayani kote kuhakikisha wametimiza Malengo ya kufikisha asilimia 100 ambapo kwa sasa wamefikia asilimia 78.
Hata hivyo Mwenda amesema kuwa kila shule,iwe ya sekondari au Msinginiblazima ilime hekari zisizopungua mbili za alizeti au mahindi kwa ajili ya chakula cha wanafunzi Shuleni.
Aidha amewataka wazazi na walezi kupelela chakula na michango yote ya chakula Shuleni ili watoto waendelee kupata uji na chakula cha mchana Shuleni amesema hiyo ni lazima na wala siyo hiyari ya mzazi au Mlezi.
Mwenda amesema amesema mpaka sasa shule 68 kati ya 108 zinahudumia chakula kwa wanafunzi Shuleni na zilizobakia bado hazitoi huduma hiyo,Amehimiza kufanya hivyo mara moja iwezekanavyo.
Sanjari na hayo,Mkuu wa wilaya amewataka Watendaji wote kushirikiana na walimu kuhakikisha wanaboresha na kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti maeneo yote ya shule, barabaraza shule na kuhakikisha miti hiyo inakua ili kutekeleza agizo la makamu wa Rais Dkt. Philip Isidory Mpango alilolitoa hivi karibuni katika Uzinduzi wa upandaji Kitaifa.
0 comments:
Post a Comment