METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, January 29, 2023

POLISI MAKALA YAWATOA HOFU WANANCHI IKIADHIMISHA POLICE COMMUNITY DAY

Mkuu wa Polisi Mkalama SSP Richard Mwaisemba akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama Amony Sanga wakizungushia Vijiti kwenye mti uliopandwa kuashiria utunzaji wa mti ili ukue.



SGT Khaim Sekelela   askari kutoka Mkalama akipanda mti.

Zoezi la upandaji miti likiendelea 

E9184 SGT Chiganga Polisi Mkalama Akipanda mti kwenye siku ya Police Community Day hapo jana.

Mwananchi Stephano Aroni akishiriki zoezi la upandaji miti 

Mkuu wa Polisi wilaya ya Mkalama SSP Richard Mwaisemba akipanda mti katika kijiji cha Tumuli.

G4823 CPL Peter  polisi wa Mkalama Akipanda mti.

Kaimu Mtendaji wa Kata ya Tumuli Bi.Amina Omary akimsikiliza kaimu Mkurugenzi wa Mkalama Amony Sanga Wakazi wa zoezi la Upandaji miti. 

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama Amony Sanga Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Milade baada ya kushiriki zoezi la upandaji miti hapo jana.

Wananchi na iguguno wakishiriki zoezi la upandaji miti 

Afisa Mazingira Wilaya Mkalama Amony Sanga ambaye alimkaimisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Mkalama Akipanda mti pembezoni mwa uwanja uliopo karibu na kituo cha polisi Iguguno. 


Mwananfunzi akiwa amebeba mti kushiriki zoezi la upandaji miti katika vijiji vya Tumuli,Milade na Iguguno.



Na Hamis Hussein - Mkalama, Singida

JESHI la Polisi Wilaya ya Mkalama limewaongoza wananchi Wilayani Humo Kupanda miti 250 katika Kijiji cha Tumuli na Milade vilivyopo kata ya Tumili ikiwa ni maadhimisho ya siku ya police community yenye lengo la kushiriki shughuli za kijamii kama vile kufanya usafi wa mazingira na kusaidia wahitaji.

Akizungumzia siku hiyo iliyofanyika hapo Jana January 28 2023 Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkalama Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Richard Mwaisemba amesema siku ya Police Community imelenga kuliweka pamoja jeshi hilo la polisi na wananchi ili kushiriana katika mambo mbalimbali ya kijamii hivyo akatumia wasaa huo kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kubaini wahalifu kwenye jamii.

"Siku hizi polisi sio adui wa wananchi, ndio maana leo tumeshirikiana nao katika siku hii ya police Community day ambayo huwaleta polisi pamoja na wananchi kufanya kazi za Kijamii kwahiyo tuendelee kushirikiana ikiwemo kwenye Masuala ya Kufichua Wahalifu Mwenye Jamii", Alisema SSP Mwaisemba.

SSP Mwaisemba aliongeza kwa kuwataka wananchi hao kutunza miti iliyopandwa ili iwe na tija kwao na vizazi vijacho.

"Hii miti muitunze vizuri ili iwe faida baada ya kukua, mtapata vivuri, Matunda, lakini hewa itakuwa nzuri sana".

Kwa upande wake Afisa Mazingira wa Wilaya ya Mkalama Amony Sanga akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema Maelekezo ya Kitaifa ya upandaji Miti ni kuwa Kila wilaya inatakiwa kupanda miti isiyopungua Milioni 1 na Laki tano (1500000) hivyo akawasisitiza wananchi kutumia jitihada binafsi katika kufanikisha zoezi hili.

"Maelekezo ya kitaifa yanasema kila Wilaya inatakiwa kupanda miti isiyopungua Milioni 1.5 hivyo mtaona jinsi gani tuna kazi kubwa ya kufanya , kwahiyo ndugu wananchi mjitahidi hata kutumia jitiahada Binafsi ili tufanikishe zoezi hili", Alisema Sanga.

Sanga Alisema kuwa bado miche ya miti inaweza isitoshe kwenye Zoezi hilo hivyo akaahidi kuwashirikisha wakala wa huduma za Misitu TFS  ili kuongeza miti itakayopandwa kwenye maeneo mbalimbali.

Kaimu Mtendaji wa Kata ya Tumuli Amina Omary ametaja umuhimu wa zoezi hilo  kuwa ni pamoja na kuzuia mmomonyoko wa udongo na kutengeneza madhari na hewa itakayotumiwa na viumbe hai wakiwemo wanandamu.

Pamoja na kutaja umuhimu huo Mtendaji huyo alieleza kuwa ili kuhakikisha miti hiyo inakuwa na faida tajika inapatika kama kata watakuwa wanatoa elimu ya utunzaji mazingira ya miti hiyo kukua vizuri na akaahidi kumwagia miti pindi mvua zitakapopungua au kuisha kabisa.

Hii ni awamu ya Tatu ya Upandaji miti katika Halmashauri hiyo ambapo mpaka sasa tayari jumla ya miche ya miti elfu 15000 imegawiwa na Wakala wa Huduma za Misitu TFS kwaajili ya upandaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kwenye shule, Taasisi za dini na Mazingira ya Nyumbani.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com