MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda amewataka viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa kwenye mikoa mbalimbali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Ameyasema hayo
wakati wa Maadhimisho ya Miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi yaliyofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza hapo jana.
Amesema wabunge,
madiwani na watendaji wengine kuanzia ngazi ya kata wanatakiwa kushirikiana na
viongozi wa Serikali kuhakikisha fedha za miradi ya maendeleo zinatekeleza
miradi hiyo ipasavyo.
Aidha, amewataka
wanawake kuhakikisha wanaelimisha wananchi juu ya miradi mbalimbali ya
maendeleo iliyotekelezwa na Mheshimiwa Rais katika maeneo yote nchini ili wawe
na uelewa juu ya miradi hiyo.
0 comments:
Post a Comment