WAKULIMA hususani wa zao la tumbaku hapa nchini wametakiwa kuachana na dhana potofu kuhusu kilimo cha zao hilo na badala yake wafuate maelekezo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Tumbaku Tanzania (TORITA) ili kuongeza tija kwenye uzalishaji kwa faida yao na taifa kwa ujumla.
Licha ya kutozungumzwa sana lakini zao hilo linatajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa kutokana na fedha za kigeni na kwa mujibu wa Taasisi hiyo kwa mwaka 2021 zao la Tumbaku liliingiza Taifa fedha za kigeni dola milioni 127.5 na kuendelea kuwa na mchango mkubwa hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dr. Jacob Lisuma Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Tumbaku Tanzania (TORITA) anasema tangu kuanzishwa kwa TORITA kumekuwa na msaada mkubwa kwa wakulima hali iliyosababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la Tumbaku.
0 comments:
Post a Comment