METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 4, 2023

MAAFISA KILIMO WATAKIWA KUWAFIKIA WAKULIMA MASHAMBANI KUWATATULIA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI

Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba akizungumza na Maafisa na wataalamu wakilimo na viongozi wengine katika ziara yake  ya kikazi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Singida.


Afisa kilimo wa Kata ya Mudida Dionisi Rukamba alimuonesha ukubwa wa shamba la alizeti ambalo linafanyiwa majaribio ya Mbegu na mbolea

RC Serukamba akisikiliza maelezo ya Afisa kilimo wilaya ya Ikungi akimweleze juu masuala ya Kilimo

Shamba la mahindi likiwa limeshaota

Musa Ibrahimu Mkulima wa  Mudida akiwa kwenye shamba lake mara baada ya kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Hapo jana.



Na Hamis Hussein - Singida

MAAFISA na wataalamu wa kilimo Mkoani Singida wametakiwa kuwafikia wakulima kuwaelewesha njia za kilimo cha kisasa  kitakachoendana na mabadiliko ya Hali ya Hewa sanjari na kuwasaidia  namna  bora ya  kukabiliana na viwavijeshi  kwenye mazao wakati huu uzalishaji wa kilimo ukiendelea.

Hatua hiyo inajiri mara baada ya Ziara ya mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba kukagua vituo vya Kufanyia majario ya mbegu za mazao ya kimkakati katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Ikungi na msisitizo ukiwa ni kuwaelimisha wakulima kubadilisha mfumo wa ulimaji.

RC Serukamba alisema lengo la kuzisha viwavi Source center nikuangalia aina gani ya mbolea itafaa katika mazao ya aina Fulani ili matokeo yake yakiwa mazuri yatakuwa msaada kwa wakulima maeneo ya vijijini ambako uzalishaji unafanyika hivyo akawataka wataalamu wakilimo wakiongozwa na Maafisa Kilimo kufika mashambani kuwasaidia wakulima kulima kitaalamu pamoja na matumizi sahihi ya Mbolea.

“Nia ya kuanzisha hivi Viwavi Center ni kukabiliana na changamoto zinazowakumba wakulima na tumegawanya maeneo vipande vipande ili kuona mbolea gani itatumika kwenye mazao Fulani ambapo matokeo yake ndio yataanza kutumiwa na wakulima”. Alisema RC Serukamba

Serukamba Aliongeza kuwa wataalamu wa kilimo wasijifungie maofisi wakawatelekeza wakulima pekee yao kipindi hiki cha uzalishaji hivyo waendelee kufika mashambani kuwasaidia utaalamu wa kilimo chenye tija hasa matumizi ya mbolea, Madawa na namna ya kupalilia.

“Lazima mue mnakuja kuwasidia kuangalia maendeleo watu wakatavyopanda, watakapopalilia, nivuzri sana muendelee kuleta utaalamu msiwache pekee yake ili matokeo mazuri yatayopatikana yatumike kwa wakulima wote”, Aliongeza RC Serukamba.

Kuhusu suala la Wakulima kulima zao moja RC Serukamba aliwataka maafisa kilimo kuwaelimisha wakulima hayo kugawa mashamba ili waweze kulima mazao tofauti tofauti kuliko kuamini zao moja ambalo hali ya hewa ikibadiliza mavuno yanakuwa chini.

Diwani wa kata ya Mudida Omary Mande alimweleza mkuu wa mkoa Serukamba kuwa changamoto inayopelekea wakulima wengi katika halmshauri hiyo kushindwa kutumia mbolea ni umbali wa kuifuata   mbolea hiyo hivyo akaomba wakulima wasogezewe huduma hiyo.

Mande Alisema kuwa wakulima wengi wa Halmashauri ya Singida wako mbali na vituo  inapopatikana mbolea  jambo linalowapa wakati mgumu sana na wengine kukata tamaa kabisa ya kutumia mbolea kwenye mashamba yao.

Kufuatia kilio hicho cha Diawani wa MUdida RC Serukamba alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida kulitatua haraka suala hilo

“Kumwambia Mkulima aende kule afuate mbolea ni mbali hivyo angalieni namna ya kuwafikishi mbolea kwenye maghala yao na msiwache pekee yao nanyi muende kule, kwa kuwa na mbole ya kupandia hatukupata nzuri Mkurugenzi aleteeni hata ya kukuzia”. Alisema Serkamba

Afisa kilimo kata ya Mudida  Dionisi Rukamba alimweleza mkuu wa mko Serukamba kuwa wakulima wengi wana Imani kuwa ukipanda mapema alizeti haita zaa inayotakiwa jambo ambalo  afisa huyo alisema wanaendelea kuwapa elimu,

Musa ibrahimu Mkulima wa Alizeti na Mahindi alisema kuwa changamoto kubwa wanayokutana nayo kwa sasa ni Viwavijeshi ambavyo vinashambulia mazo hivyo akaiomba serikali ya mkoa wa Singida kuwaangalia wakulima hao kwa kuwapatia madawa  pamoja na pembenjeo.

 

 

 

 

 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com