METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 15, 2017

Madaktari wakubaliana na serikali ya Kenya kumaliza mgomo

media
Madaktari nchini Kenya wakiwa na mabango kushinikiza kusikilizwa wakati walipoandamana hivi karibuni jijini Nairobi. 

Serikali ya Kenya na madaktari hatimaye wamefikia makubaliano ya kumaliza mgomo, makubaliano ambayo pande zote mbili zilitia sahihi. Hatua hii inakuja baada ya mgomo wa madaktari kudumu siku mia moja. Mgomo ambao umeathiri vibaya huduma za afya nchini Kenya.

Hata hivyo, mzozo ambayo ulisababisha mgomo haukupatiwa ufumbuzi, amesema Dk Ouma Oluga, mkuu wa chama cha madaktari nchini Kenya.

Chama cha madaktari kikiongozwa na mwenyekiti wake Oroko Samuel, kuliungana na Waziri wa Afya Cleopha Mailu kwenye ofisi za magavana wakati wa kutiwa sahihi makubaliano hayo.

Makubaliano hayo yalitiwa sahihi mbele ya viongozi wa kidini.

Madaktari walikua wakidai utekelezaji wa mkataba uliosainiwa pamoja na serikali mwaka 2013. Mkataba huo unaeleza kwamba mshahara wa sasa unapaswa kuongezwa mara tatu.

Makubaliano pia yalipanga kuwaajiri madaktari zaidi na kutoa vifaa bora kwa hospitali za umma.
Katika miezi ya hivi karibuni, majaribio kadhaa ya kumaliza mgomo yalishindwa.

Madaktari 5,000 wa sekta ya umma walishiriki katika mgomo huo.

Hospitali nchini Kenya zilikua zimeanza kuwafuta kazi madaktari wanaogoma na kuwaondoa kutoka nyumba zao.

Huduma kwenye hospitali za umma zilikua zimetatizika kutokana na mgomo ambao ulianza mwezi Disemba, huku madaktari na wahudumu wengine wa afya wakitaka mshahara zaidi na mazingira bora ya kufanya kazi.

Itafahamika kwamba serikali ya Kenya ilikua ilipeleka madaktari wa kijeshi kwenye hospitali kubwa zaidi nchini humo ya Kenyatta, baada ya madaktari wa mwisho 300 waliokuwa wakifanya kazi kujiunga na mgomo uliokua ukiendelea nchini kote.RFI
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com