![]() |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Marry Masanja akiwa katika picha ya pamoja na matumishi wa wizara hiyo idara ya Habari baada ya kufanya kikako january 3 2023. |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amewataka Maafisa Habari,Uhusiano na Mawasiliano wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuongeza kasi ya kutangaza vivutio vya utalii ili kuifungua Dar es Salaam kiutalii.
Hatua hiyo ni
kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia
Suluhu Hassan za kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour.
Naibu Waziri Masanja
ameyasema hayo January 3 2023 mara baada ya kukutana na Maafisa Habari katika
kikao kazi kilichofanyika kwenye Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS) jijini Dar es Salaam.
Alisema ni
lazima kuifungua Dar es Salaam kiutalii kwa kuwa ndio lango kuu la kupokelea
wageni kutoka nchi mbalimbali duniani.
“Lazima kila
mwezi tuwe na tukio la kiutalii jijini Dar es Salaam na tufanye kwa
kushirikiana hivyo ni jukumu la kila taasisi kuhakikisha inatangaza vivutio
vyote bila kubagua taasisi nyingine” alisema Naibu Waziri Masanja. Na kuongeza
kwa kusema
“Taasisi zote za
Wizara ya Maliasili na Utalii zinatunza, zinahifadhi na zinaendeleza utalii
hivyo tunachotakiwa kufanya ni kumuunga mkono Mheshimiwa Rais ili kile
alichokianzisha kilete matokeo chanya.”Mhe. Masanja amesisitiza.
Amewataka
maafisa hao kutenga bajeti za kutangaza vivutio vya utalii vya maeneo yao ya
kazi kupitia vipeperushi na kuviweka katika maeneo yanayotembelewa na wageni.
“Vipeperushi
vinatakiwa vionekane katika maeneo yote ambayo watalii wanafika hapa jijini Dar
es Salaam kama hoteli, viwanja vya ndege na magari yanayobeba abiria “madereva
taxi” wanaopokea watalii ili kuvutia watalii wengi zaidi. Vipeperushi hivyo
viwe na vivutio vyote vya utalii vya maeneo yote ya taasisi za Wizara ambazo ni
TAWA, TANAPA, TFS na MAKUMBUSHO YA TAIFA.
Sambamba na hilo
amezitaka taasisi za Wizara hiyo kuitumia fursa ya meli inayoleta watalii
nchini kwa kutangaza ujio wake kwa kualika waongoza watalii kushiriki katika
kuwapokea na kuwatembeza katika vivutio mbalimbali vilivyoko jijini Dar es
Salaam.
Naibu Waziri Masanja
amehitimisha kikao hicho kwa kuwataka maafisa hao kuisemea Wizara kwa nguvu
moja ili kufikia malengo ya kuongeza idadi ya watalii nchini.
0 comments:
Post a Comment