METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, January 23, 2023

CCM YAZINDUA KAMPENI YA KUIKIJANISHA KATA YA KILIMANI-DODOMA


Na Barnabas Kisengi, Dodoma

Chama cha Mapinduzi Kata ya kilimani kimezindua kampeni kabambe ya kuikijanisha kilimani kuwa ya kijani kwa upandaji miti zaidi ya mia sita katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali ambayo yatajengwa shule ya msingi secondary, kituo cha afya, kituo cha Polisi, soko, ofisi za Chama cha Mapinduzi tawi la chinyoyo na Ofisi ya Serikali ya mtaa Chinyoyo katika kata hiyo. 

Akizindua zoezi hilo la kuikijanisha kilimani Naibu waziri wa kilimo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la dodoma Mhe Anthony Peter Mavunde amesema uwepo wa maeneo hayo ya taasisi mbalimbali za serikali kutaipelekea kilimani kuwa ya kijani kwa kupanda miti katika maeneo hayo.

Naibu waziri Mavunde amesema lengo la kuikijanisha kilimani na Dodoma kwa ujumla ni kuunga mkono jitihada za maagizo ya Makamu wa RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha Dodoma unarudi katika hali yake ya zamani ya kijani na kuhakikisha inaboresha Mazingira ili vizazi vijavyo vije kunufaika na mazingira

"Tukiangalia maeneo haya kwakweli tumeharibu Mazingira zamani hapa ulikuwa msitu mzuri unao vutia laikini sasa kwa kuwa tumekuwa tukifanya shughili za kibinadama kama kulima, kukata kuni na uchomaji wa mkaa tumeharibu haya mazingira hivyo Sasa kwakuwa tumeamua kurudisha hali hii ya kuikijanisha Kilimani basi tuhakikushe hii miti tunaitunza ili pindi tutakapo anza Ujenzi wa taasisi hizi kuwe na miti ya kutosha ili tupate vivuli na kuzuia umomokanyaji wa udongo katika maeneo haya"Alisisitiza waziri Mavunde

Aidha Waziri Mavunde akiwataka viongozi wa mtaa Mwenyekiti wa mtaa wa chinyoyo na Mtendaji wa Mtaa kuhakikisha wanashirikiana kuhakikisha miti yote iliyopandwa inatunzwa na ikibidi watumie sheria ndogondogo za Halimashauri ya Jiji kuwabana watu wanaokuwa wanaharibu Mazingira Ili kuhakikisha wanaeakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili wachukuliwe hatua.

Kwa Upande Wake Diwani wa Kata ya kilimani Mhe Neema Mwaluko amesema wamepanda miti zaidi ya mia sita ikiwemo miti ya kivuli na matunda katika maeneo hayo ya taasisi za serikali na zoezi hilo litakuwa endelevu hadi Kilimani iwe ya kijani.

Naye Katibu wa Siasa na uwenezi kata ya kilimani Fatuma Hassan amesema wao kama Chama cha Mapinduzi Kata ya kilimani wanatimiza malengo ya ilani ya Chama hicho kwa kuhakikisha wanaikijanisha Kilimani katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo na kuwataka wanachama wa Chama hicho kuonyesha mfano katika kupanda miti na kuitunza katika maeneo yao yote.

Faustina Bendera ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa chinyoyo amesema katika kuunga mkono jitihada za maagizo ya Makamu wa RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philipo Mpango la kutunza Mazingira wao wameanza na maeneo ya taasisi hizo na kuwataka Wananchi wote kuhakikisha wanatunza Mazingira na kila mwananchi aliyepanda mtii Katika maeneo hayo ya taasisi ahakikishe anatunza mtii wake hadi ukuwe.

"Pamoja na kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali pia kila kaya inatakiwa kupanda walau miti minne ya matunda na kivuli na hili tutalisimamia na Wajumbe wangu wa serikali ya Mtaa kuhakikisha tutakagua kila kaya maana tunayo miti ya kutosha ambayo tumepatiwa na Chama cha Mapinduzi Kata ya kilimani hivyo ni wajibu Wetu kuhakikisha tunaendela kusimamia swala hili la utunzaji wa Mazingira na kuifanya Kilimani kuwa ya kijani" amesema Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa chinyoyo Faustina Bendera

Zoezi hilo la uzinduzi wa upandaji miti zaidi ya mia sita zilihudhuriwa na Wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi na mashirika mbalimbali yanayotunza Mazingira kama chapakazi na Leadd foundation na Wadau mbalimbali wa Mazingira na viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma Mjini.

Mwisho
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com