Na Doreen Aloyce, Dodoma
MHADHIRI Msaidizi wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Roggers Ndyonabo amesema kuwa chuo hicho Kimekuwa kikifanya tafiti kuhusu masuala ya uendeshaji wa mashauri ya watoto na wamebaini kuwa yapo mahitaji wanayotakiwa kupewa waendeshaji wa mashauri ya Watoto.
Akiongea na waandishi wa habari katika ufunguzi wa wiki ya Mahakama jijini Dodoma Mhadhiri huyo amesema baada ya Kutoa utafiti uliofadhiliwa na shirika la watoto duniani (UNICEF) tulipata picha juu ya mahitaji yanayotakiwa wapewa waendeshaji wa mashauri ya watoto kuwa wanaotakiwa kupewa elimu endelevu.
Aidha Mhadhiri Ndyonabo amesema baada ya kubaini hali hiyo waliweza kupata fursa ya kutoa kozi endelevu kwa wadau wote wanaoshughulika na mashauri ya Watoto Kama vile mahakimu mawakili wa serikali, mawakili wakujitegemea, wadau wa haki jinai polisi na Magereza .
" Niukweli kwamba wadau wanaoshughulika na Masuala ya mashauri ya Watoto wanaotakiwa kupata mafunzo ya Mara kwa Mara ili waweze kufanya kazi zao kwa weledi," amesema Mhadhiri Ndyonabo .
Na kuongeza Kusema"Katika Masuala yote ya haki jinai lazima kuwepo na muendelezo wa mafunzo juu ya haki za Watoto na ndipo weledi utakapoonekana," amesema
Pia amesema wamefanya utafiti kwenye Masuala ya migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Tanga na mikoa mingine lengo likiwa ni kuangalia namna ya kuweza kutatua na kusuluhisha migogoro hiyo na kutoa ushauri kwa Kutoa miongozo na kuzindua miongozo ya kutatua migogoro hiyo.
Hata hivyo ameeleza Chuo kinatoa mafunzo ya Sheria kwa ngazi mbalimbali kwa kozi ndefu na fupi ambapo kwa kozi ndefu na fupi wanatoa Astashahada ya sheria na stashahada ya sheria, kwa Watumishi wa mahakama.
0 comments:
Post a Comment