METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, July 15, 2022

CCM YACHAGUA VIONGOZI WA MAPINDUZI SPORTS KLABU

IMG-20220715-WA0097
Msimamizi wa Uchaguzi wa Mapinduzi Sports Club Wilson Nkambaku Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa Uchaguzi huo .
IMG-20220715-WA0100

Msimamizi wa Uchaguzi wa Mapinduzi Sports Club Wilson Nkambaku akiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kumalizika kwa Uchaguzi huo jijini Dodoma

Na Mwandishi wetu DODOMA

WATUMISHI wa chama cha Mapinduzi (CCM) makao makuu na Jumuiya zake wamepiga kura ya kuchagua viongozi ambao wataiongoza Mapinduzi Sports klabu.

Viongozi waliochaguliwa ni Mwenyekiti,makamu mwenyekiti, katibu mkuu katibu mkuu msaidizi, mweka hazina mjumbe wa mkutano mkuu na wajumbe wa kamati tendaji.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Mapinduzi Sports Club Zakayo Kishiwi ilieleza kuwa katika uchaguzi huo wajumbe wamemchagua Kajoro Vyohoroko kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo,Annael Samweli Makamu mwenyekiti, na Neema Mfugale kuwa katibu Mkuu.

“Viongozi wengine waliochaguliwa ni katibu msaidizi Jumanne Mzee na Eunice Malya amechaguliwa kuwa mweka hazina.

Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwa wajumbe walimchagua Hamis Hilali kuwa mjumbe wa mkutano mkuu na kuwapitisha wajumbe wa kamati tendaji ambao ni Bushuru Mohamed, Elizabeth Muhina, na Marry Ngerangera.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa mwenyekiti huyo aliahidi kuifufua mapinduzi sports klabu kivingine katika michezo yote .

“Uchaguzi wa viongozi hao ulifanyika Julai 8 mwaka huu katika ukumbi wa NEC uliopo CCM makao makuu chini ya usimamizi wa wa mwenyekiti wa uchaguzi Wilson Nkambaku,”amesema
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com