Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia kwenye Kongamano la UWT la kumpongeza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji
wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi lililofanyika kwenye hotel ya
Verde. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwenyekiti wa UWT Taifa Mhe. Gaudensia Kabaka
akihutubia kwenye Kongamano la
UWT la kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.
Dkt. Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi lililofanyika kwenye hotel ya Verde. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais)
Sehemu ya Waliohudhuria Kongamano la UWT la
kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali
Mohamed Shein kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi
lililofanyika kwenye hotel ya Verde. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na
wanawake kwa ujumla kuchapa kazi zaidi na kushikamana katika kuleta maendeleo
kwa jamii nzima.
Makamu wa Rais ameyasema hayo kwenye Kongamano la
Wanawake la Kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kutekeleza ilani ya Uchaguzi
ya Chama cha Mapinduzi lililofanyika kwenye hoteli ya Verde, wilaya ya
Magharibi A, mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
“Sisi ni sehemu muhimu sana ya utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, hivyo Kongamano hili liwe chachu yetu
katika kuchapa kazi zaidi”alisema
Makamu wa Rais.
Aidha, aliwasihi wanawake kuchukua jukumu la
kuzisemea na kuzitangaza kwa sauti kubwa kazi nzuri zinazofanywa na
viongozi wa Serikali zetu mbili ili wananchi wazijue na
wasipotoshwe.
“Sote ni mashuhuda wa kazi kubwa na nzuri
iliyofanyika hapa Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitatu. Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar chini ya Uongozi mahiri wa Dokta Shein imefanya kila liwezekanalo
kuboresha hali ya maisha ya wananchi wa Zanzibar kupitia miradi mbalimbali ya
maendeleo katika sekta zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi.”Alisisitiza Makamu wa Rais.
Mheshimiwa Rais Shein ametekeleza kwa umahiri
mkubwa ilani ya Uchaguzi na kuweza kuleta mafanikio makubwa katika Uimarishaji
wa Huduma za afya, Elimu , ujenzi wa miundombinu,Kilimo, ufugaji, uvuvi na
Ushirika, kuwawezesha Wazee, wanawake na Walemavu na kuwateua
wanawake kwenye nafasi za Uongozi.
Makamu wa Rais ameupongeza uongozi wa UWT Taifa
pamoja na Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar kwa kuandaa kongamano hilo
ambalo sit u la kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Shein kwa kazi kubwa aliyofanya kwa
kipindi cha miaka mitatu, bali Kongamano la kutoa ushuhuda kwa wananchi kuhusu
kazi nzuri inayofanywa na Chama Cha Mapinduzi katika kusimamia maendeleo ya
wananchi.
Mawaziri wa SMZ , Wawakilishi wa Viongozi na Naibu
Waziri wa Nishati kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano walipata nafasi ya
kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Kongamano
hilo.
Kongamano hili lilifanyika Pemba tarehe 9, Machi
2019 ambapo lilitanguliwa na ziara liyoanza tarehe 6-8 mwezi Machi 2019 na
ziara kama hiyo imefanyika Unguja kuanzia tarehe 11-14 Machi 2019 ambapo tarehe
15 Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa ilikutana.
0 comments:
Post a Comment