METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 20, 2022

WATU WENYE ULEMAVU WAOMBA KUPEWA KIPAUMBE KWENYE AJIRA

Makamu Mwenyekiti Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) mkoa wa Iringa Leo Sambala akiongea wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali uliondaliwa na shirika lisilo la kiserikali la IDYDC na kufadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa Inclusive Media Project unaofadhiliwa na Internews Tanzania

Na Fredy Mgunda,Iringa. 

CHAMA cha walemavu mkoa wa Iringa kimeiomba Serikali kuwapatia upendeleo wa ajira pindi zinvyotangazwa ili nao waweze kupata ajira hizo kwa kuwa wanauwezo wa kufanya kazi kama watu wengine na itasaidia kutatua changamoto ya kukosekana kwa ajira kwa watu wenye ulemavu nchini Tanzania. 

Akizungumza na waandishi wa habari Makamu mwenyekiti chama cha walemavu Tanzania (CHAWATA),Iringa Rukia Makweta alisema kuwa moja ya adhima nzima za elimu jumuishi ni kuanda taifa la watu wenye mahitaji maalaumu na walemavu ambao si tegemezi kwa kuwaandaa kujiajiri na kuajiriwa.

Makweta alisema kuwa muda mrefu nchini Tanzania kumekuwa na dhana kuwa mlemavu ni mtu anayepaswa kuwa tegemezi katika jamii jambo ambalo si kweli. 

Alisema kuwa baadhi ya watu huenda mbali zaidi na kuwaficha watu wenye ulemavu ili wasionekane na jamii kiasi cha kuwakosesha fursa za kijamii na kiuchumi ikiwemo elimu na mitaji,ajira.  

Makweta alisema kuwa licha ya kuwa nyuma katika fursa mbalimbali kutokana na mitazamo hasi ya jamii dhidi yao, idadi ya watu wenye ulemavu wanaojitosa katika shughuli za kiuchumi Tanzania imezidi kuongezeka kwa kasi ndani ya miaka saba iliyopita. 

Kwa upande wake Katibu wa wa shirikala watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) mkoa wa
Iringa Leo Sambala alisema kuwa ripoti ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi ya mwaka 2020/21 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya takwimu (NBS), inabainisha kuwa idadi ya watu wenye ulemavu wenye ajira imeongezeka hadi takriban theluthi mbili au asilimia 63.2 mwaka 2020/21 kutoka asilimia 59.1 mwaka 2014. 

Sambala alisema kuwa inamaanisha hadi mwaka jana takriban watu sita kati ya 10 wenye ulemavu walikuwa na ajira ama kwa kujiajiri au kuajiariwa. 

Katika kipindi hicho, kiwango cha watu wenye ulemavu wenye umri miaka 15 na zaidi ambao hawakuwa na ajira nacho kilishuka. Takwimu hizo zinaeleza zaidi kiwango cha watu wenye ulemavu mwaka 2020/21 kilikuwa asilimia 6,nusu ya kile kilichokuwepo mwaka 2014 ambacho kilikuwa asilimia 12.4. 

Kwa nyakati tofauti serikali imekua  inawahamasisha walemavu kuchangamkia fursa za ajira zinazotangazwa na serikali kwa sababu ni wachache wanaojitokeza ikiashiria Mwamko mdogo  wa walemavu katika uombaji wa ajira.serikali inasisitiza kwamba endapo  mtu mwenye ulemavu au mahitaji maalumu atakua ametimiza vigezo bila kuogopa changamoto zinazowakabili kuomba ajira hizo kwani mchakato wote wa maombi ya ajira unafanywa kwa kufuata kanuni na Sheria za Nchi ambayo inampa kila mtu haki ya kupata ajira, 

Alisema kuwa sheria namba 9 ya Ajira ya mwaka 2010 inasema,“Mwajiri yoyote awe wa Umma au Binafsi mwenye waajiriwa kuanzia 20 na kuendelea lazima asilimia 3 ya waajiriwa hao iwe kwa ajili ya watu wenye ulemavu” hii inaonyesha kuwa walemavu wana haki ya kuajiriwa mahali popote. 

Lakini Sambala alisema kuwa ni vyema walemavu kuzitaja changamoto zao kweye fomu za maombi ili serikali iweze kuwaandalia mazingira rafiki kwa ajili ya mchakato mzima wa upatikanaji wa ajira na baada ya kupata ajira waweze kupangiwa sehemu ambazo hazitakua changamoto kwao. 

Aidha Serikali inawapa kipaumbele walemavu kuanzia wakati mchakato wa usajili hadi wakati wa kupanga ajira hivyo basi walemavu wenye vigezo vilivyoanishwa kwenye matangazo ya ajira wajitokeze kutuma maombi ya nafasi hizo. 

Walemavu wanahaki kisheria hivyo waachane na mawazo ya kudhani wakitaja changamoto zao kwenye maombi hawatapatiwa nafasi. 

Sambala alisema kuwa Serikali inatambua nafasi ya Walemavu katika kuchangia maendeleo ya Nchi na ina wahamasisha kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kujikwamua kiuchumi. 

katika kutambua umuhimu wa vyombo vya habari Iringa Development of youth disabled and children care(IDYDC) shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa Inclusive Media Project  unaofadhiliwa na internew Tanzania  katika mkoa wa Iringa kupitia Mratibu wa  mradi Reuben Magayane alisema kuwa vyombo vya habari vinapaswa kusema kuwasemea watu wenye ulemavu ili waweze kuapata ajira kama watu wengine. 

Magayane alisema kuwa waandishi wa habari na vyombo vya habari vinaweza kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kufikisha ujumbe moja kwa moja kwa serikali husika.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com