MKUU wa Wilaya ya Kahama Mhe Fadhil Nkulu
MKUU wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Fadhil Nkulu amewataka Wanaume walizaa nje ya ndoa mjini hapa kuhakikisha kuwa wanawatunza watoto wao waliozaa nje ya ndoa, kama wanavyowatunza waliozaa ndani ya ndoa katika familia zao.
Aliyasema hayo juzi katika kilele cha Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo kimkoa ilifanyika katika Kata ya Mwendakulima katika Halmashauri ya mji wa Kahama na kuongeza kuwa kwa sasa ofisi yake itahakikisha kuwa inawatafuta watu hao.
Alisema kuwa wazazi wenye tabia kama hiyo ya kuzaa nje na kuwatelekeza watoto wao wanatambulika katika ofisi na kuongeza kuwa hali hiyo haitavulimiwa na watoto ambao wanawatambua wazazi wao lazima warudishwe kwao.
“Haiwezekani kwa mwanaume mzima uzae nje ya ndoa na kisha kuacha kumtunza mwanao hali inachangia kwa kiwango kikubwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu huku wazazi wao wakiwepo tu,” alisema Nkurlu.
Mkuu huyo wa Wilaya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ZainabTelack aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, alisema Mkoa wa Shinyanga una jumla ya watoto 54,352 wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuongeza kuwa hali hiyo inachangiwa na mambo mengi.
0 comments:
Post a Comment