METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, April 9, 2022

WALIMU 490 WA MASOMO YA BIASHARA WA SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI NA ZISIZO ZA SERIKALI WAPATIWA MAFUNZO

 

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Dr Lyabwene Mtahabwa akizunungmza wakati  ufunguzi wa  mafunzo kazini kwa walimu wa masomo ya Biashara na ufundi yanayofanyika  katika Chuo cha ADEM  cha Bagamoyo mkoani Pwani.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Dr Lyabwene Mtahabwa akisoma hotuba kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu sayansi na teknolojia Prof Eliamani Sedoyoka jana April 8 2022 Kwenye ufunguzi wa mafunzo

Mafunzo ya walimu yakieendelea kutolewa na kaimu katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na Teknolojia Dr. Lyabwene Mtahabwa

Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba akizungumza katika mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo wakifurahia  maelekezo ya kaimu katibu mkuu.

Na Mwandishi wetu , Pwani

SERIKALI  imewataka walimu wa shule za sekondari nchini wanaofundisha masomo ya Biashara kuweka umakini katika kuwajengea wanafunzi Uwezo, maarifa, stadi na mitazamo chanya ya maisha kupitia masomo wanayoyafundisha.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Dr Lyabwene Mtahabwa wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu sayansi na teknolojia Prof Eliamani Sedoyeka jana April 8 2022 Kwenye ufunguzi wa mafunzo kazini kwa walimu wa masomo ya Biashara na ufundi yanayofanyika  katika Chuo cha ADEM  cha Bagamoyo mkoani Pwani.

Hotuba hiyo ilisisitiza kuwa utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi utawezekana ikiwa taifa litakuwa na walimu waliondaliwa vyema  kwa kupata mafunzo stahiki yatakayomuwezesha kumjenga mtoto kiakili, kimwili na kimtazamo na kuwa na umahiri wa kukabiliana na mazingira yake na hasa  katika kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye maisha ya kila siku ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira.

"Ni matumaini yangu kuwa uboreshaji wa ufundishaji na ujifunzaji si kwamba  utaleta tija kwa walimu tu, bali  utaleta pia matokeo chanya kwa wanafunzi".alisema Dr  Mtahabwa

Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba naye alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaimarisha  walimu wa masomo ya  biashara ( Book Keeping na Commerce)  kuutekeleza mtaala kwa ufanisi.

"Matokeo ya mafunzo ni kuwa walimu watatumia mbinu bora za ufundishaji na ujifunzaji. Vilevile, mafunzo haya yanaimarisha walimu katika njia bora za upimaji wa umahiri". Alisema Dkt. Komba.

Dkt. Komba aliongeza kuwa  jumla ya walimu 980 wa shule za  sekondari za serikali na zisizo za serikali watapatiwa mafunzo katika masomo ya michepuo amapo Kundi la kwanza litakuwa ni masomo ya biashara (Commerce na Book Keeping) , Kundi la pili ni walimu 90 wa masomo ya ufundi, Kundi la tatu litakuwa la walimu 400 wa masomo ya Sayansikimu na Kilimo.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dkt. Charles Msonde alisema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha walimu hao kupata ujuzi wa namna ya utungaji wa maswali yanayozingatia ujenzi wa umahiri.

Mafunzo hayo Yanayotolewa kwa ushirikiano wa watalaamu kutoka TET, vyuo vikuu, vyuo vya ualimu na Baraza la Mitihani Tanzania yanafanyika kwa siku sita ambapo  yameanza tarehe  8  na yanatizamiwa kumalizikia tarehe  13 ya  mwezi  huu  April  2022.

 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com