Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Dr Lyabwene Mtahabwa akisoma hotuba kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu sayansi na teknolojia Prof Eliamani Sedoyoka jana April 8 2022 Kwenye ufunguzi wa mafunzo |
Mafunzo ya walimu yakieendelea kutolewa na kaimu katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na Teknolojia Dr. Lyabwene Mtahabwa |
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba akizungumza katika mafunzo hayo. |
Washiriki wa mafunzo wakifurahia maelekezo ya kaimu katibu mkuu. |
Na Mwandishi wetu , Pwani
SERIKALI imewataka walimu wa shule za sekondari nchini wanaofundisha masomo ya Biashara kuweka umakini katika kuwajengea wanafunzi Uwezo, maarifa, stadi na mitazamo chanya ya maisha kupitia masomo wanayoyafundisha.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Dr Lyabwene Mtahabwa wakati akisoma hotuba
kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu sayansi na teknolojia Prof Eliamani
Sedoyeka jana April 8 2022 Kwenye ufunguzi wa mafunzo kazini kwa walimu wa
masomo ya Biashara na ufundi yanayofanyika
katika Chuo cha ADEM cha Bagamoyo
mkoani Pwani.
Hotuba hiyo ilisisitiza kuwa utoaji wa elimu bora kwa
wanafunzi utawezekana ikiwa taifa litakuwa na walimu waliondaliwa vyema kwa kupata mafunzo stahiki yatakayomuwezesha
kumjenga mtoto kiakili, kimwili na kimtazamo na kuwa na umahiri wa kukabiliana
na mazingira yake na hasa katika kutatua
changamoto zinazojitokeza kwenye maisha ya kila siku ikiwa ni pamoja na ukosefu
wa ajira.
"Ni
matumaini yangu kuwa uboreshaji wa ufundishaji na ujifunzaji si kwamba utaleta tija kwa walimu tu, bali utaleta pia matokeo chanya kwa
wanafunzi".alisema Dr
Mtahabwa
Mkurugenzi Mkuu
wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba naye alisema kuwa lengo la
mafunzo hayo ni kuwaimarisha walimu wa
masomo ya biashara ( Book Keeping na
Commerce) kuutekeleza mtaala kwa
ufanisi.
"Matokeo
ya mafunzo ni kuwa walimu watatumia mbinu bora za ufundishaji na ujifunzaji.
Vilevile, mafunzo haya yanaimarisha walimu katika njia bora za upimaji wa
umahiri". Alisema Dkt. Komba.
Dkt. Komba aliongeza kuwa jumla ya walimu 980 wa shule za sekondari za serikali na zisizo za serikali
watapatiwa mafunzo katika masomo ya michepuo amapo Kundi la kwanza litakuwa ni
masomo ya biashara (Commerce na Book Keeping) , Kundi la pili ni walimu 90 wa
masomo ya ufundi, Kundi la tatu litakuwa la walimu 400 wa masomo ya Sayansikimu
na Kilimo.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania,
Dkt. Charles Msonde alisema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha walimu hao kupata
ujuzi wa namna ya utungaji wa maswali yanayozingatia ujenzi wa umahiri.
Mafunzo hayo Yanayotolewa kwa ushirikiano wa watalaamu
kutoka TET, vyuo vikuu, vyuo vya ualimu na Baraza la Mitihani Tanzania
yanafanyika kwa siku sita ambapo
yameanza tarehe 8 na yanatizamiwa kumalizikia tarehe 13 ya mwezi huu April
2022.
No comments:
Post a Comment