Na Asila Twaha, Arusha
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde amewataka Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa taarifa na takwimu sahihi za elimu ili kuboresha usimamizi wa elimu.
Akizungumza hayo jana Jijini Arusha wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Umoja wa Maafisaelimu wa Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara(REDEOA) lengo likiwa ni kujifunza, kubadilishana uzoefu na namna ya kuzitatua changamoto katika utendaji kazi wa shughuli za kielimu.
Katika mkutano huo Mhe. Silinde amewataka viongozi hao kusimamia miradi ya elimu na kuwepo na taarifa na takwimu sahihi za kielimu ili elimu inayotolewa iendane na uhitaji wa sehemu husika. Aidha, amewaelekeza viongozi hao kuzitatua changamoto zinazo ikabili sekta ya elimu.
Amesisitiza kusimamia suala la uandikishaji kwa wanafunzi wa darasa Awali na Kwanza Mhe. Silinde amesema bado ni changamoto amezielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa wakiwemo wasimamizi wa elimu kuhakikisha wanasimamia suala la uandikishwaji wa wanafunzi ili watoto wapate elimu. “Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu imeidhinisha fedha kiasi cha shilingi bilion 304 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ya kufundishia na kujifunzia amesema ni vyema watoto wapate elimu ili Taifa liwe na wataalam wengi na bora.
Vilevile ameeleza kuhusu azma ya Serikali ya kuendelea kuajiri walimu na kuendelea kuboresha maslahi yao amewataka wasimamizi hao kufanya kazi kwa waledi katika utoaji na kusimamia walimu. Akizungumzia ununuzi wa magari ya Maafisaelimu Sekondari amesema magari hayo yameshaagizwa na taratibu zitakapokamilika hivi karibuni watakabidhiwa amesema hayo yote ni katika kuboresha sekta ya elimu ili waweze kusimamia.
“Nimeridhishwa na kauli mbiu hii ya “Kuboresha Miundombinu ya Shule ni Kuimarisha Elimu kwa Maendeleo endelevu na Kukuza Uchumi wa Taifa” kauli mbiu inaendana na malengo na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa adhma yake ni kuhakikisha, kuendeleza elimu bila malipo na kuboresha miundombinu ya elimu”. amesema Mhe. Silinde
Aidha, nitoe msisitizo kwa wasimamizi wa elimu kuhakikisha kuwa walimu na wanafunzi wanahudhuria darasani kila siku kulingana na ratiba za masomo zilivyopangwa ili kuepuka kuathiri utekelezaji wa Kalenda za mtaala.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe akitumia mkutano huo kwa kuwapongeza maafisa hao kwa usimamizi wa madarasa 15000 ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO – 19, na kuwaelekeza Wakurugenzi kuendelea na usimamizi wa fedha za Serikali na kupanga bajeti vizuri ya fedha za mapato ya ndani ili kujenga na kuendeleza ujenzi wa matundu ya vyoo mashuleni.
Kwa upande wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro amewahakikishia watumishi wote wa Umma kuwa, usimamizi wa haki za watumishi utaendelea kwa kuzingatiwa Sheria, Taratibu za Utumishi wa Umma na kuelezea mfumo wa uhamisho kwa walimu na watumishi unafanyiwa kazi hivi karibu utakuwa tayari kutumika na kabla ya kutumika kutakuwa na mafunzo ili kuwe na uwelewa katika kuufanyia kazi katika kutenda haki amesema hii itasaidia mgawanyo sawa kwa watumishi sehemu za kazi.
0 comments:
Post a Comment