Mkuu wa mkoa wa singida Dkt. Binilith Mahenge wapili kutoka kushoto , Mwenyekiti wa ccm mkoa wa singida Alhaj Juma Kilimba wapili kutoka kulia , Yohana msita Mjumbe wa halmashauri kuu taifa kwa mkoa wa kwanza kulia na singida Lucy Boniface katibu wa ccm wa kwanza kushoto wakiwa katika kikao cha halmashauri kuu ya chama kilichofanyika janury 22 mjini singida.
Mwenyekiti wa ccm
alhaj juma kilimba akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya ccm katika
ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa
Wakuu wa wilaya ,
wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali wakifuatilia kikao cha halmashauri kuu
Ndugu Francis Isaack (Mb)
wa iramba mashariki akichangia kwenye kikao cha halmashauri kuu juu ya suala la
ukopeshaji wa mbegu kwa wakulima.
Ndugu Miraji Mtaturu (Mb) wa singida mashariki
akichangia kwenye kikao cha halmashauri kuu ya ccm singida
Elia Digha mwenyekiti
wa Halmashauri ya Singida akiuliza
msimamo wa serikali juu ya utunzaji rasilimali za halmashauri hiyo.
Wajumbe wakisikiliza
hoja zikitolewa kwenye kikao.
Na Nathaniel Limu -
SINGIDA
CHAMA Cha Mapinduzi
(CCM) mkoani Singida kimempongeza mwenyekiti wa CCM taifa ambaye ni Rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kumteua
Dk.Tulia Ackson kugombea nafasi ya spika wa Bunge kufuatia kujiudhuru kwa aliyekuwa spika ndugu Job Ndugai.
Pongezi hizo
zimetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na kamati kuu ya CCM mkoa wa Singida,kwenye kikao cha
kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika kipindi cha kuanzia
julai hadi desemba mwaka jana (2021).
Kamati hiyo imesema
uteuzi huo ni sahihi ikizingatiwa Dk.Tulia ana uzoefu wa muda
mrefu katika kuliongoza bunge kwa ufanisi mkubwa na kuwaomba
wabunge wa singida walihudhuria kikao hicho kwenda kumpigia kura Dk Tulia ili
aweze kuliongoza bunge tukufu.
“Ninyi wabunge wetu wa
mkoani kwetu,nendeni mkatuchangulie kwa kura zote Dk.Tulia,ili ashinde kwa
kishindo.Mteule wetu uwezo anao tena mkubwa tu.Imani yetu kwake ni kwamba
atasimamia bunge kikamilifu, ili muhimili huo utekeleze majukumu yake kwa
ufanisi”,amesema
Alhaj Kilimba.
Kwa upande wa ilani ya
uchaguzi,mwenyekiti huyo alisema chama kinaipongeza serikali ya mkoa wa Singida
chini ya uongozi thabiti wa mkuu wa mkoa Dkt.Binilith Mahenge Kwa utekelezaji
wake wa ilani ya uchaguzi kwa kiwango kilichokusudiwa.
Akifafanua,alisema
kuwa katika miradi yote ya sekta mbalimbali iliyotembelewa na kamati za siasa
za wilaya na mkoa,miradi hiyo imetekelezwa kama ilivyokusudiwa.Na ina thamani
ya fedha zilizotumika.
“Miradi kama ya ujenzi
wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari,ipo vizuri sana na
inavutia.Hongereni sana, na kipekee pongezi nyingi ziende kwa mkuu wa mkoa Dkt.Mahenge”,amesema mwenyekiti
huyo.
Pia Alhaj
Kilimba,alitumia nafasi hiyo kumshukru Rais Samia kwa uamuzi wake wa kuupatia
mkoa wa Singida, fedha nyingi zilizotosha kugharamia miradi mbalimbali.
”Sisi wasaidizi wako
na Watanzania kwa ujumla,tutaendelea kukuombea kwa Mwenezi Mungu akupe nguvu na
afya njema, ili uendelea kuwatumikia vema Watanzania wenzako”.aliongeza alihaji
kilimba mwenyekiti ccm singida
Kwa upande wake mkuu
wa mkoa wa Singida,Dkt.Mahenge alisema kuwa katika kipindi hicho,mkoa umepokea
zaidi ya shilingi 13.4 bilioni kupitia UVIKO-19 kwa ajili ya kujenga vyumba vya
madarasa 330 kwa shule za sekondari na 332 vya shule za msingi.
Alisema vyumba hivyo vya madarasa vimekamilika kwa wakati
na vina viti,meza na madawati ya kukidhi mahitaji .
“Katika kipindi cha
utekelezaji ,mkoa umepokea jumla ya shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya
kutekeleza miradi ya ukarabati,upanuzi na ujenzi wa miundo mbinu mbali mbali
katika vituo vya afya 11 kupitia tozo”,alisema mkuu huyo wa mkoa.
Dkt.Mahenge alisema
pamoja na mafanikio mengi waliyopata katika kipindi hicho,vile vile
walikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa watumishi, kuchelewa kwa
baadhi ya vifaa vya ujenzi wa miradi ya elimu na bei ya bidhaa kupanda.
Naye katibu tawala
mkoa wa Singida,Doroth Mwaluko,ameahidi kabla ya jumatano wiki hii,taarifa juu
ya stofahamu ya fedha zaidi ya 660 milioni za zao la korosho,itakuwa
imefahamika.
Wakati huo huo,katibu
CCM mkoa wa Singida,Lucis Boniface,alisema katika miradi yote mkoani
waliyoikagua,hawajapata dosari yo yote.Amewapongeza wakuu wa wilaya ya
watendaji wengine waliosimamia miradi hiyo.
Aidha,alisema ujenzi
wa daraja la Misingi wilaya ya Mkalama,kazi inaendelea vizuri.Kamati ilitatua
mgogoro wa ujenzi wa kituo cha afya Mkalama, na sasa kazi ya ujenzi wa kituo
hicho inaendelea.
Awali kikao hicho
kilisimama kwa dakika moja,kumkumbuka na kumwombea mwalimu sekondari Luluma
wilaya ya Iramba,Simon Anthony, aliyeuawa na mke wake
Mwanaisha Shamiru,kwa kuchomwa moto.
0 comments:
Post a Comment