METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, October 26, 2017

SHIRIKA LA HAKI ELIMU YASHIRIKIANA NA JAMII KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU

 Mkurugenzi
wa Shirika lisilo la kiserikali la
 Haki Elimu
nchini John Kalage akipanda mti katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii
iliyoambatana na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya
sekondari ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na
wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu jana (Habari Picha Na Pamela Mollel,Arusha)
 
 Wafanyakazi
wa shirika la Haki Elimu nchini wakiongozwa na Mkurugenzi wao John Kalage wa
tatu kushoto, wakichimba shimo kwaajili ya kuhifadhi taka ngumu katika shule ya
Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii
 
 
Wafanyakazi
wa shirika la Haki Elimu nchini wakijiandaa kwenda kupaka rangi madarasa katika
shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii
  Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipongezwa na Mkuu wa shule hiyo Vitalis Nada mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti katika shule hiyo jana
 
Mmoja
wa wazazi shuleni hapo akishiriki 
zoezi la umwagiliaji wa maua
katka maadhimisho ya huduma kwa jamii iliyoratibiwa na Shirika na Haki Elimu

Wafanyakazi
wa Haki Elimu wakiwa wananendelea na zoezi la upakaji rangi shule hapo jana
Aliyeshika
ndoo nyekundu ni Abraham Lazaro kutoka  Idara ya Habari na uchechemuzi akiwa na
mfanyakazi mwenzake wakiendelea na zoezi la umwagiliaji  katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo
Mkoani Arusha katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii

 

Mwanafunzi
shuleni hapo akiwa amebeba ndoo kwaajili ya kubebea maji kwaajili ya shughuli ya
umwagiliaji shuleni hapo jana
 
Meneja Idara
ya Huduma, fedha na Utawala Daniel Luhamo akichimba shimo la kuhifadhia taka
ngumu shuleni hapo

Mfanyakazi
wa Haki Elimu Raphael akiendelee na shughuli ya upakaji rangi
 
Rose
Mwenda Mmoja wa wafanyakazi wa HakiElimu kutoka Idara ya Ushiriki na
Uwajibikaji wa jamii akipaka rangi bati katika shule ya
Mukulat iliyopo Mkoani Arusha


 
Mwanafunzi
wa kidato cha nne shule ya Sekondari  Mukulat
Stella Massawe akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa HakiElimu John Kalage,
zawadi  iliyotengeneza katika klabu yao
ya wanafunzi ya Njoo Tuzungumze
Mkuu wa
Miradi HakiElimu – Boniventura Godfrey akibeba ndoo za kuchotea maji kwaajili
ya umwagiliaji

Baadhi ya
wazazi wakisalimia katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana
na uapandaji wa miti na tunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya
mukulati iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa
shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu


Afisa Elimu
Taaluma Halmashauri ya Wilaya Arusha Vijijini ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa
Halmashauri   akimkabidhi zawadi iliyotolewa na bodi ya
shule kwa Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini John Kalage kwa kutambua umuhimu wa
elimu Nchini
 Picha ya pamoja
 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com