Baadhi ya washiriki wa Kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita wakifatilia kwa makini mada mbalimbali zikiwasilishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza wakati wa kongamano katika maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Mchambuzi na mshauri wa sera katika Wizara ya kilimo Ndg Revelian Ngaiza Akiwasilisha mada kuhusu mchango wa sera za kilimo katika mageuzi ya uchumi wa viwanda wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Meneja wa Muendelezo wa wakulima wadogo TADB Ndg Joseph Mabula Akiwasilisha mada kuhusu Mikopo nafuu kwa mapinduzi ya kilimo na viwanda wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Afisa uendeshaji Mwandamizi Utoaji Mikopo na kudai madeni Kutoka Mfuko wa Pembejeo Ndg Joshua Kalab akiwasilisha mada kuhusu Mchango wa mfuko wa pembejeo katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kupambana na njaa na kupunguza umasikini hususani vijijini wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini kutoka Wizara ya Kilimo Ndg Issa Sabuni akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Katibu wa Chama cha Biashara Tanzania Mkoa wa Kagera (TWCC) Bi Paskazia Sebastian akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Afisa Mfawidhi kutoka Taasisi ya udhibiti wa mbegu TOSCI Mkoa wa Mwanza Ndg Ngura Joseph Akiwasilisha mada kuhusu Mchango wa mbegu bora katika usalama wa chakula wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Afisa Kilimo Mkuu kutoka Wizara ya kilimo Bi Mwanaid Kiya Akiwasilisha mada kuhusu Sumu kuvu kwenye mahindi: Madhara katika sekta ya kilimo, Biashara na afya ya binadamu wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Zikiwa zimesalia siku mbili kufikia kilele cha
maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambapo maadhimisho hayo huanza Octoba 10
kila mwaka na kufikia ukomo Octoba 16, wadau mbalimbali kutoka sekta ya kilimo
na nyinginezo wameshiriki Kongamano la Maadhimisho ya chakula lililofanyika
katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Katika
kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga
aliwasisitiza wataalamu wa kilimo kuwasaidia wakulima nchini ili kuongeza
ufanisi katika kilimo kutoka katika kilimo kwa ajili ya chakula pekee badala
yake na kuwa na kilimo tija kwa ajili ya chakula na biashara.
Alisema
kuwa ili kuongeza ufanisi na kukuza soko la mazao ya chakula na biashara nchini
watanzania wanatakiwa Kuwa wazalendo na kupenda vyakula vitokanavyo na mazao
mbalimbali yanayozalishwa nchini.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Geita aliwapongeza wadau mbalimbali
walioshiriki katika Kongamano hilo ambao ni Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo
na Uvuvi, Vikundi vya wajasiriamali, Makampuni ya simu, na Shirika la umeme Tanzania
TANESCO ambapo alisema kuwa imani yake kuwa kongamano hilo litaibua chachu
katika uzalishaji wa kilimo na uhifadhi bora wa chakula.
Alisema kuwa umuhimu wa kongamano hilo unaakisi Kaulimbiu ya maadhimisho ya
Chakula duniani kwa mwaka 2017 isemayo “Badili mwelekeo wa uhamaji; Wekeza katika usalama wa chakula na maendeleo
Vijijini” ikiwa ni sehemu ya ubashiri wa kutokea mzozo mkubwa
wa chakula.
Alisema jukumu muhimu la kilimo cha familia katika
kuangamiza njaa na umaskini ni kuhakikisha kuna usalama wa upatikanaji wa
chakula na lishe bora, kuboresha kipato, kusimamia vyema rasilimali, kuyalinda
mazingira na kufanikisha maendeleo endelevu, hususani katika maeneo ya mikoani.
Katika Kongamano hilo mada mbalimbali ziliwasilishwa
ikiwemo Mada ya Mchango wa sera ya kilimo katika magaezi ya uchumi wa viwanda,
Mikopo nafuu kwa mapinduzi ya kilimo na viwanda, Mchango wa mfuko wa pembejeo
katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kupambana na njaa na kupunguza umasikini
hususani vijijini.
Mada zingine rafiki katika kongamano hilo ni pamoja
na Mchango wa mbegu bora katika usalama wa chakula, Umuhimu wa kilimo cha mazao
ya mizizi kwa kuboresha lishe na kipato cha jamii, sumu Kuvu kwenye mahindi
(Madhara katika sekta ya kilimo, Biashara na afya ya binadamu), Msingi wa uhuru
wa kiuchumi na Tanzania ya Viwanda sambamba na Ufugaji nyuki unaoongeza
mavunoya asali na kipato katika kaya.
Akiwasilisha mada kuhusu mchango wa sera za kilimo
katika mageuzi ya uchumi wa viwanda Mchambuzi na mshauri wa sera kutoka Wizara
ya kilimo Ndg Revelian Ngaiza Alisema
kuwa Sera ya Taifa ya kushajiisha uwekezaji ya mwaka 1996 na Sheria ya
uwekezaji ya mwaka 1997 imeiweka sekta ya kilimo kama sekta kiongozi katika
uchumi hivyo Sekta hiyo imeendelea kuwa uti wa mgongo katika kukuza uchumi kwa
kipindi cha kati na cha muda mrefu.
Alisema kuwa Serรก ya
Taifa ya kilimo ya mwaka 2013 ilidhamiria Kuwezesha kuwepo mabadiliko ya sekta
ya kilimo kuwa kilimo cha kisasa, kibiashara na sekta yenye ushindani ili
kuhakikisha usalama wa chakula na upunguzaji wa umaskini kutokana na ongezeko
la uzalishaji wa mazao yenye ubora.
Aliendelea kusema kuwa katika Serikali ya
Awamu ya tano kumekuwa na mikakati na programu mbalimbali ambazo zimetekelezwa
na kuchangia kikamilifu katika kukuza kilimo na hifadhi ya jamii. Alitaja
programu na mikakati ambayo ni Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDS) wa
mwaka 2002; na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP I) ya mwaka 2006.
Ngaiza alisema Mabadiliko
ya ukuaji wa sekta ya kilimo hadi kufikia kuchangia kwa kiasi kinacho ridhisha
katika ukuaji wa uchumi wa Viwanda na upunguzaji wa umaskini bado kunahitajika
juhudi za kila mdau miongoni mwao ni Serikali, wakulima, sekta binafsi,
wanataalum n.k ili kutimiza azma hiyo.
Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya
Chakula Duniani hapa nchini Tanzania Kitaifa yatafikia ukomo tarehe 16
Oktoba 2017 katika Viwanja vya CCM Kalangalala, ambapo mgeni rasmi atakuwa
Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Dkt Charles Tizeba.
Maadhimisho ya kwanza ya siku hii yalianza mwaka 1981. Hivyo maadhimisho ya
mwaka huu ni ya 36 na yanasherehekewa kwa pamoja na maadhimisho ya miaka 72 ya kuanzishwa kwa FAO tarehe 16
Oktoba, 1945.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment