Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa imeanza kikao leo Jumapili 15/10/2017 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Mhe Sadifa Juma Khamis (MCC/MB)
Kikao hiki ni cha kawaida cha kikanuni ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia na kufanya mapendekezo ya wagombea nafasi mbali mbali kwa ngazi Taifa na Mikoa.
Kikao hiki cha siku mbili ni maandalizi ya kikao cha Baraza Kuu la UVCCM Taifa kitakachofanyika Jumanne 17/10/2017 mjini Dodoma, vilitanguliwa na kikao cha Secretariat ya Baraza kuu Taifa kilichofanyika juzi jijini Dar Es Salam.
Kauli yetu ni: Kulinda na Kujenga Ujamaa
Jokate U. Mwegelo
Kny: Katibu Mkuu
15/10/2017
0 comments:
Post a Comment