METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, November 29, 2021

SHIRIKA LA WOTE SAWA MWANZA LATOA MAFUNZO KWA WAAJILI NA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI



Shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa majumbani na kupinga usafirishaji haramu wa Binadamu hasa mtoto la jijini Mwanza (WOTE SAWA) Kwa Ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania limeendesha mafunzo kwa wafanyakazi wa majumbani na waajili wao.

Akizungmza na Wazo huru Blog Mratibu wa mradi huo Bi Demitila Faustine kutoka shirika la Wote sawa alisema mradi huo wa miezi mitatu unatekelezwa katika   kata hiyo ukihusisha mitaa michache na kwa kuanza walikutana na waajili wa wafanyakazi hao.

“ Tuko hapa Nyasaka katika kutekeleza mradi huu ujulikanao kama Vunja Ukimya linda haki za mfanyakazi wa nyumbani na Nyasaka ni moja ya eneo la Mradi na tulikutana na waajili ambao wengi wao ni walimu wa shule za Msingi Nyasaka na Muungano pamoja na sekondari ya Nyasaka.” Alisema Demitila

Aidha alisema kuwa kwa siku mbili kuanzia tarehe 24 na 25 waliwafahamisha kuhusu  haki na wajibu, wao kama waajili wana wajibu gani kwa wafanyakazi wao lakini pia ni sheria zipi ambazo zinamlinda mtoto mfanyakazi wa nyumbani na namna ya kusuluhisha migogoro inayotokea sehemu za kazi na nini kifanyike.

“ Tuliwafahamisha  waajili kuhusu  vitu vya kuzingatia wakati wanataka kuajili mfanyakazi wa nyumbani pamoja na umuhimu wa mikataba ya kazi na tuliona muitikio mkubwa kwani wengi wa waliohudhuria  waliomba tuwapatie mikataba hiyo.” Aliongeza Bi Demitila

Alisema baada ya mafunzo hayo waajili hao waliomba wafanyakazi wao nao wapewe mafunzo ili wafahamu hayo mambo kwa undani Zaidi  ili watakapoenda kusaini mikataba na wafanyakazi wao kuwe na uelewa wa pamoja kuhusu vipengele vilivyopo kwenye mikataba hiyo.

“ Tarehe  27 na 28 tulikutana na wafanyakazi wao  na kuwapa mafunzo na Kupitia mafunzo haya tunaenda  kuwa na jamii ya wafanyakazi ambayo itakuwa salama na hakuna ukatili dhidi yao kwani kwa siku hizi mbili tuliwafundisha mambo mbalimbali ikiwemo kutunza mali za familia, kuheshimu mwaajili yake na kutimiza wajibu wake.” Aliongeza kusema Bi Demitila

“ Tumekutana na wafanyakazi wa nyumbani 50 wa kata hii ya Nyasaka tumewaelimisha kuhusu haki zao na wajibu wao lakini pia tumewaambia wasiwe wanajifungia tu ndani  wanaweza kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii  ingawa bado ni waajiliwa wa kazi nyingine.” Alisema Bi Demitila

Akizungumzia siku 16 za kupinga ukatili Bi Demitila aliiasa jamii kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake akisema kuwa hata wafanyakazi wa majumbani nao ni wafanyakazi kama wafanyakazi wengine kwani ukatili wa aina yoyote kwao haukubali.

Kwa upande wao wafanyakazi waliohudhuria mafunzop hayo walilishukuru sana Shirika la Wote sawa na Shirika la Women Fund Tanzania kwa  mafunzo hayo kwani wamejifunza mambo mengi, ikiwemo haki na wajibu wao kama wafanyakazi.

“ Kabla sijapata haya mafunzo ya Wote sawa nilikuwa sijui chochote kuhusu wafanyakazi wa majumbani lakini kupitia mafunzi haya nimejifunza mambo mengi ikiwemo haki na wajibu wa mfanyakzi wa ndani, nawashukuru Wote sawa nimeelewa.” Alisema Josephine Bahati

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com