Shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa majumbani
na kupinga usafirishaji haramu wa Binadamu hasa mtoto la jijini Mwanza (WOTE
SAWA) Kwa Ufadhili wa Shirika la Women Fund Tanzania limeendesha mafunzo kwa
wafanyakazi wa majumbani na waajili wao.
Akizungmza na Wazo huru Blog Mratibu wa mradi huo Bi
Demitila Faustine kutoka shirika la Wote sawa alisema mradi huo wa miezi mitatu
unatekelezwa katika kata hiyo ukihusisha mitaa michache na kwa
kuanza walikutana na waajili wa wafanyakazi hao.
“ Tuko hapa Nyasaka katika kutekeleza mradi huu
ujulikanao kama Vunja Ukimya linda haki za mfanyakazi wa nyumbani na Nyasaka ni
moja ya eneo la Mradi na tulikutana na waajili ambao wengi wao ni walimu wa
shule za Msingi Nyasaka na Muungano pamoja na sekondari ya Nyasaka.” Alisema
Demitila
Aidha alisema kuwa kwa siku mbili kuanzia tarehe 24
na 25 waliwafahamisha kuhusu haki na
wajibu, wao kama waajili wana wajibu gani kwa wafanyakazi wao lakini pia ni
sheria zipi ambazo zinamlinda mtoto mfanyakazi wa nyumbani na namna ya
kusuluhisha migogoro inayotokea sehemu za kazi na nini kifanyike.
“ Tuliwafahamisha
waajili kuhusu vitu vya
kuzingatia wakati wanataka kuajili mfanyakazi wa nyumbani pamoja na umuhimu wa
mikataba ya kazi na tuliona muitikio mkubwa kwani wengi wa waliohudhuria waliomba tuwapatie mikataba hiyo.” Aliongeza
Bi Demitila
Alisema baada ya mafunzo hayo waajili hao waliomba
wafanyakazi wao nao wapewe mafunzo ili wafahamu hayo mambo kwa undani Zaidi ili watakapoenda kusaini mikataba na
wafanyakazi wao kuwe na uelewa wa pamoja kuhusu vipengele vilivyopo kwenye
mikataba hiyo.
“ Tarehe 27
na 28 tulikutana na wafanyakazi wao na kuwapa
mafunzo na Kupitia mafunzo haya tunaenda
kuwa na jamii ya wafanyakazi ambayo itakuwa salama na hakuna ukatili
dhidi yao kwani kwa siku hizi mbili tuliwafundisha mambo mbalimbali ikiwemo
kutunza mali za familia, kuheshimu mwaajili yake na kutimiza wajibu wake.”
Aliongeza kusema Bi Demitila
“ Tumekutana na wafanyakazi wa nyumbani 50 wa kata
hii ya Nyasaka tumewaelimisha kuhusu haki zao na wajibu wao lakini pia
tumewaambia wasiwe wanajifungia tu ndani
wanaweza kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii ingawa bado ni waajiliwa wa kazi nyingine.”
Alisema Bi Demitila
Akizungumzia siku 16 za kupinga ukatili Bi Demitila
aliiasa jamii kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake akisema kuwa hata
wafanyakazi wa majumbani nao ni wafanyakazi kama wafanyakazi wengine kwani
ukatili wa aina yoyote kwao haukubali.
Kwa upande wao wafanyakazi waliohudhuria mafunzop
hayo walilishukuru sana Shirika la Wote sawa na Shirika la Women Fund Tanzania
kwa mafunzo hayo kwani wamejifunza mambo
mengi, ikiwemo haki na wajibu wao kama wafanyakazi.
“ Kabla sijapata haya mafunzo ya Wote sawa nilikuwa
sijui chochote kuhusu wafanyakazi wa majumbani lakini kupitia mafunzi haya
nimejifunza mambo mengi ikiwemo haki na wajibu wa mfanyakzi wa ndani,
nawashukuru Wote sawa nimeelewa.” Alisema Josephine Bahati
No comments:
Post a Comment