Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB) imeandaa
kongamano kubwa litakalowakutanisha
wanawake wafanyabiashara , wajasiliamali, waajiriwa, waliopo vyuoni wateja wa benki hiyo na wasio wateja kwa lengo
la kumfanya mwananmke kujitambua kuwa
yeye ana wajibu mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa.
Akizungngumza Oktoba 15, 2021 katika kipindi cha
Morning Express kinachorushwa na City Fm Radio 90.5 ya Jijini Mwanza Meneja
masoko na mawasiliano wa Benki hiyo makao makuu Grace Majige amesema kwa
kutambua mchango mkubwa wa mwanamke kuanzia
ngazi ya familia kama kusomesha wameona waandae kongamano hilo ambalo mwanamke
atajifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wanawake wenzake.
“ Kila mmoja anatambua mwanamke ana mchango mkubwa
sana tangia ngazi za familia lakini pia
hela anayopata mwananmke uwa inarudi nyumbani hivyo sisi kama benki tunataka kumsaidfia
mwanamke ajifunze mengi kutoka kwa wenzie lakini pia ajue kama ana mchango
mkubwa sana kwenye taifa hili.” Amesema
Aidha amewataka wanawake wa Mwanza kuhudhuria kongamano hilo kwani ni fursa pekee na muhimu
kwa kila mmwanamke anayependa kushiriki katika kukuza uchumi wa Taifa na ambaye
anapenda kujifunza kwani siku hiyo watawasikia wanawake mbalimbali ambao wataelezea hatua, changamoto na mambo
mbalimbali waliopitia mpaka kutimiza ndoto zao.
Kwa upande wake meneja wa Tawi la TCB lililopo Pamba
Alex Minai amesema mbali na kongamano hilo Benki hiyo ya Serikali imekuwa ikitoa huduma mbalimbali ikiwemo
mikopo ya vikundi, mteja wa biashara ya
katikati, mteja mkubwa na makampuni.
“Kuna akaunti za vikundi, watu binafsi, za makampuni
, za vikundi ambayo operesheni yake ni bure kabisa na katika kuelekea siku ya
jumatatu tarehe 18 tuna akaunti maalumu kabisa kwa ajili ya wanawake
inayojulikana kama tabasamu imbayo ipo kwa ajili ya mtu mmoja au kwa vikundi na
siku hiyo ya kongamano tutawafungulia akaunti kwa watakaokuwa tayari.” Amesema
Aidha amesema anawakaribisha wanawake wote wa Mkoa
wa Mwanza lakini watakaoshiriki ni wale
tu ambao wamepewa mwaliko na kwa wale ambao bado hawajapata mwaliko wanatakiwa kufika na kujisajili katika mojawapo ya matawi yao
yanayopatikana eneo la Liberty, Pamba na Kenyata
“Tungependa tuwe na wanawake wote lakini kwa sababu
ya ufinyu wa eneo watakaohudhuria ni wale waliopewa mwaliko tu na ili uweze
kushiriki fika katika matawi yetu uweze kujisajili kwani siku hiyo kuna vitu
vizuri sana ambavyo vimeandaliwa na benki yetu. ” Amesema
Naye afisa kutoka kitengo cha bima Makao makuu Emmanuel
Kaganda amesema mafunzo mbalimbali
yatatolewa kama namna ya ukuzaji wa
biashara pamoja na kutumia changamoto kama fursa na hii ni maalumu kwa wale
ambao wakianzisha biashara inapokwama kidogo
tu huamua kuachana nayo.
“ Watu wengi wana ndoto ya kufungua na kuanzisha
biashara mfano kufuga nk, sasa wengi ikitokea labda ameanza kufuga na ikitokea mfugo
wake umekufa anaamua kuacha sasa kupitia mafunzo haya tunaamini tutazalisha
wafanya biashara wasiokata tamaa.” Amesema
Benki ya Serikali ya Biashara (TCB) ni muunganiko wa
benki ya Maendeleo (TIB) na benki ya Posta (TPB) ambayo ilizinduliwa julai 15,
2021 na Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba
ikiwa ni jitihada za serikali kujenga uchumi imara na shindani.
Kongamano hilo lenye kauli mbiu ”nafasi ya mwanamke katika kukuza uchumi wa Taifa” litafanyika katika ukumbi wa Rocky City Mall Mwanza Oktoba 18, 2021 kuanzia saa 1:30 asubuhi ambapo Zaidi ya wanawake 400 wanatarajiwa kuhudhuria.
0 comments:
Post a Comment