METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 16, 2021

DKT MABULA APONGEZA JITIHADA ZA SERIKALI YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI


Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini Mhe Rais Samia Suluhu Hassan za kuendelea kukamilisha miradi ya kimkakati ikiwemo ule wa ujenzi wa daraja la Busisi maarufu kama daraja la Magufuli.

Dkt Mabula amefafanua hayo wakati wa muendelezo wa ziara yake ya kiwizara  katika mikoa ya Kanda ya ziwa ukiwemo Mwanza na Geita alipopita katika daraja la Busisi ambapo amesema kuwa ukamilishaji wa miradi ya kimkakati utasaidia kuiongezea nchi mapato sambamba na kurahisisha huduma Kwa wananchi hivyo kitendo kinachofanywa na Serikali ya Rais Samia ni kitendo Cha kupongezwa na kuungwa mkono na Wananchi wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi za kisiasa au nyenginezo

'.. Tumpongeze Mhe Rais Samia na Serikali yake Kwa kuamua kuendelea na ukamilishaji wa miradi ya kimkakati, Miradi hii itasaidia kuongeza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla ..' Alisema

Aidha Mhe Dkt Mabula amewaasa wananchi waliojirani na miradi hiyo ya kimkakati kuhakikisha wanaitunza na kushirikiana na wakandarasi katika kutekeleza miradi hiyo Ili iweze kukamilika Kwa wakati na kuleta tija Kwa taifa

Katika mkoa wa Mwanza miradi mbalimbali ya kimkakati imeendelea kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa jengo la abiria na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, ujenzi wa reli ya kisasa SGR, ujenzi wa vivuko katika Ziwa Victoria, ujenzi wa daraja la Busisi, ujenzi wa stendi za kisasa(Nyamhongolo na Nyegezi) na ujenzi wa masoko ya kisasa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com