Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa pamoja na viongozi wengine wa
Kitaifa wakishiriki Misa ya Dominika ya 17 ya Mwaka ‘A’ wa Kanisa Katoliki
pamoja na Kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa
katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mjane wa
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa Mama Anna
Mkapa akiwasili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Misa
ya Dominika ya 17 ya Mwaka ‘A’ wa Kanisa Katoliki pamoja na Kumuaga Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa.
Gari la
Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba Jeneza lenye mwili wa Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa wakati likiwasili
katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Makanali
wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu
Marehemu Benjamin William Mkapa wakati wakiingia katika sehemu ya Ibada katika
Misa ya Dominika ya 17 ya Mwaka ‘A’ wa Kanisa Katoliki pamoja na Kumuaga Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam.
Mjane wa
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Mzee Benjamin William Mkapa Mama Anna
Mkapa akiwa pamoja na familia yake katika Misa hiyo iliyofanyika katika Uwanja
wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment