Baadhi ya wadau wa Utalii wakiwa katika kikao kazi cha kupitia mkakati wa huduma za ujirani mwema wa uhifadhi Kilichoandaliwa na Mamlaka ya usimamizi wa wanayamapori Tanzania TAWA.
Wajumbe wa kikao kazi cha kupitia mkakati wa huduma za ujirani mwema wa uhifadhi Kilichoandaliwa na Mamlaka ya usimamizi wa wanayamapori Tanzania TAWA kilichofanyika Mjini Morogoro
PICHA ya pamoja ya wadau wa Utalii wakiwa katika kikao kazi cha kupitia mkakati wa huduma za ujirani mwema wa uhifadhi Kilichoandaliwa na Mamlaka ya usimamizi wa wanayamapori Tanzania TAWA mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika Kingolwira Mkoani Morogoro makao makuu ya TAWA
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA imekutana na wadau mbalimbali wa Utalii katika kikao kazi cha kupitia mkakati wa huduma za ujirani mwema wa uhifadhi kilichofanyika katika makao makuu ya mamlaka hiyo Kingolwira Mjini Morogoro
Kikao kazi hicho kimehusisha wadau mbalimbali wa uhifadhi kama vile halmashauri za Wilaya,wadau wa maendeleo,mashirika ya uhifadhi,vyuo na watoa huduma za utalii
Akifungua Kikao kazi hicho cha siku Moja Kilichofanyika Leo July 25, 2020 Kamishna Mhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi amewaomba wadau hao wa uhifadhi kushirikiana katika kuhifadhi kwa kuwalinda wanyamapori kwa maslahi ya Taifa.
Aidha Misungwi amesema kuwa TAWA imekuwa ikichangia miradi mingi ya kimaendeleo kwa jamii inayozunguka maeneo yanayohifadhiwa na mamlaka hiyo kupitia utalii wa picha na uwindaji wa kitalii.
Sanjari na hayo amesisitiza haja ya kuweka mpango wa kushirikiana katika kudhibiti wanyamapori waharibifu
Nae Bi Gloria Bideberi msimamizi wa kitengo cha Ujirani mwema amesema kuwa fedha zilizotumwa na wadau wa utalii kwa kipindi cha mwaka 2017-2020 ni shilingi bilioni 4 fedha za kitanzania zilizotumika katika maendeleo ya jamii.
Kwa upande changamoto amesema kuwa WMA Inakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi kama vile magari na sarae za askari wa vijiji
Nao baadhi ya wadau wa TAWA wameitaka mamlaka hiyo kushirikiana katika kukabiliana na wanyamapori waharibifu wa mazao pia kusaidia vitendea kazi vya WMA kama vile mavazi na magari.
Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA imendelea kuwa mstari wa mbele katika Kuhakikisha jamii inanufaika na uhifadhi kwa maeneo wanayowazunguka kwa kusaidia miradi ya maendeleo ikiwemo,afya elimu pamoja huduma ya maji safi na salama.
0 comments:
Post a Comment