Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza
kwenye kikao cha Maafisa Madini Wakazi kilichofanyika Julai 25, 2020 katika
ukumbi wa Nguvu za Atomiki uliopo jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo
akizungumza kwenye kikao cha Maafisa Madini Wakazi kilichofanyika Julai 25,
2020 katika ukumbi wa Nguvu za Atomiki uliopo jijini Arusha.
Katibu Mkuu Madini Prof. Simon Msanjila
akizungumza kwenye kikao cha Maafisa Madini Wakazi kilichofanyika Julai 25,
2020 katika ukumbi wa Nguvu za Atomiki uliopo jijini Arusha.
Waziri wa
Madini, Doto Biteko amewapongeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwa
utendaji mzuri uliopelekea kuvuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa
fedha 2019-2020 ambapo walikusanya shilingi bilioni 528.2 ikiwa ni zaidi ya
lengo la shilingi bilioni 470 lililopangwa.
Amebainisha
kuwa ili kuendelea kufanikiwa katika kusimamia sekta ya madini viongozi wawe
tayari kujifunza na hapo ndipo watafurahia matokeo ya uongozi wao kila mmoja
katika eneo lake.
Waziri
Biteko ameyasema hayo leo tarehe 25 Julai, 2020 jijini Arusha alipokuwa
akifunga mkutano wa Katibu wa Madini, Profesa Simon Msanjila na Maafisa Madini
Wakazi wa Mikoa wenye lengo la kujadili mafanikio, changamoto na namna ya
kuzitatua kwenye Sekta ya Madini.
Wageni
wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Naibu Waziri wa Madini,
Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila,
Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi David Mulabwa, Mwenyekiti wa Tume ya
Madini, Profesa Idris Kikula, Wakuu wa Idara na Mameneja kutoka Wizara ya
Madini na Tume ya Madini.
Alisema
siri ya mafanikio makubwa katika Wizara ya Madini ni pamoja na ubunifu na
uzalendo wa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwenye ukusanyaji wa maduhuli na
kuwataka kuendelea kusimamia shughuli za uchimbaji na biashara ya madini kwa
kufuata Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake.
"Nipende
kueleza kuwa, ninatambua mchango wenu mkubwa sana kwenye ukuaji wa Sekta ya
Madini, mmekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kodi mbalimbali zinalipwa
Serikalini, hii imesaidia sana Sekta ya Madini kukua.
Katika
hatua nyingine Waziri Biteko amewataka Maafisa Madini Wakazi kutatua migogoro
kwa kusimamia Sheria na kusisitiza kuwa wasisite kuwasilisha changamoto kwa
viongozi wa Tume ya Madini pale wanapokwama.
Aidha,
aliwataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuendelea kushirikiana kwa
kubadilishana uzoefu kwenye usimamizi wa shughuli za madini ili kuongeza tija
kwenye utendaji kazi.
Naye Naibu
Waziri Nyongo akizungumza kwenye mkutano huo aliwataka Maafisa Madini Wakazi wa
Mikoa kuendelea kushirikiana kwa karibu na Wakuu wa Mikoa, Wilaya,
Taasisi nyingine pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuongeza
ufanisi kwenye utendaji kazi wao.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo
ameeleza kuwa kushikamana, kupambana na kupiga kazi ndio uwe msingi wa maafisa
hao.
Aliwataka
kila mmoja kuhakikisha anatimiza lengo la makusanyo ya maduhuli kwa mwaka wa
fedha 2020-2021 alilopangiwa ili Wizara iweze kuvuka lengo la mwaka
husika.
Naye Katibu
Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila mbali na kuwapongeza Maafisa
Madini hao aliongeza kuwa, imani kwa Serikali kwa Wizara ya Madini imeongezeka
mara baada ya kufanikiwa kukusanya maduhuli zaidi ya lengo lililowekwa awali.
"Mtakumbuka
mwaka jana tulisaini mkataba wa shilingi bilioni 10.6 na Wizara ya Fedha kwa
ajili ya kuimarisha Tume ya Madini kwa kununua vifaa mbalimbali pamoja na
magari ambapo zimezaa matunda, endeleeni kuchapa kazi na tupo tayari kuwasaidia
muda wowote."alisema Profesa Msanjila.
Wakati
huohuo, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila aliwapongeza maafisa hao na
kueleza kuwa wamesababisha wizara kuaminiwa kutokana na kukidhi vigezo baada ya
kufikia malengo ya makusanyo waliyoingia na Wizara ya Fedha mwezi Aprili, 2019
aliposaini mkataba na kupewa kiasi cha bilioni 10.6 ili kuimarisha Tume ya
Madini.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula amekiri kuwa mafanikio
yaliyopo kwenye sekta ya madini yametokana na uaminifu uliopo kwa viongozi na
watendaji wa Tume ya Madini na kuwataka maafisa hao kudumisha weledi huo wakati
wa utekelezaji wa majukumu yao.
Naye
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula aliishukuru Wizara ya Madini
kwa ushirikiano mzuri kwa Tume ya Madini hali iliyopelekea Tume kufanya vizuri
kwenye Sekta ya Madini.
Alisema
kuwa changamoto zilizoainishwa katika mkutano husika zitaandaliwa vyema na
kuwasilishwa ngazi za juu na utekelezaji wake kufanyika mara moja.
0 comments:
Post a Comment