METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 16, 2021

SHAKA:PUUZENI PROPAGANDA ZA SERIKALI KUSITISHA MPANGO WA ELIMU BILA MALIPO

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna ahadi iliyotolewa kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ambayo haitatekelezwa ikiwemo mpango wa elimu bila malipo na utatuzi wa changamoto za sekta ya elimu nchini. 

Amesema hayo wakati akikagua Ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana Nachingwea iliyopo kata ya Chiumbati mkoani Lindi.

Ndg Shaka Aliwataka wananchi wapuuze taarifa zozote za upotoshaji zinazodai serikali itasitisha mpango wa kugharamia elimu bila malipo.

Aidha amewapongeza wananchi wa kata ya Chiumbati, kijiji cha Chiumbati shuleni kwa kutoa eneo la ujenzi wa shule hiyo, kujitolea nguvu kazi na hata kuchangia ujenzi katika hatua za awali kabla ya serikali kuwaunga mkono kuendeleza ujenzi huo.

Shaka pia amewataka wananchi kujitokeza kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka 2022. Alihimiza serikali inatekeleza zoezi hilo kwani taarifa zake zina umuhimu mkubwa katika kuisaidia serikali kupanga rasilimali zake katika maendeleo ya nchi na watu wake hivyo ni muhimu kila mmoja kujitokeza kulishiriki.

Shaka yupo kwenye ziara ya Sekretarieti ya CCM Taifa inayokamilika leo mkoani Lindi ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com