METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, June 20, 2021

WAZIRI MKENDA ATOA SIKU 7 KWA MRAJIS WA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI KUREJESHA UMOJA WA VYAMA VYA MSINGI 32 VYA WAKULIMA WA KAHAWA

Waziri wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya Kahawa Tanzania uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya Kahawa Tanzania uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni.
Waziri wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya Kahawa Tanzania uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni.
Waziri wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda akikagua bidhaa mbalimbali za Kahawa wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Kahawa Tanzania uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda amempa siku 7 Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini, Dkt.Benson Ndiege  kuhakikisha anaurejesha umoja wa vyama vya msingi 32 vya wakulima wa Kahawa (G32 KNCI JVE) vinavyofanya biashara ya kahawa nchini.


Waziri  Mkenda ametoa agizo hilo kufuatia hatua ya Mrajisi wa vyama hivyo vya ushirika kuufuta umoja huo Agosti mwaka jana kwa madai ya kuwa biashara ya kahawa inapaswa kufanywa na chama cha ushirika KNCU pekee  jambo ambalo amesema sio sahihi.


Akizungumza juzi katika mkutano wa 11 wa wadau wa Kahawa uliofanyika Jijini Dodoma ambao uliwakutanisha wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya wakurugenzi, Taasisi za fedha pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama vya msingi alisema endapo akishindwa kuurejesha umoja huo hatua kali  zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kufutwa kazi.


"Kuna watu walikuwa wameungana wanajiita G32, nimempa Mrajisi wiki moja amalizane na hawa watu ili biashara ya kahawa iendelee, Kahawa ndio iliyotuletea ushirika wa kwanza hapa Tanzania na KNCU ilizaliwa kutokana na Kahawa na mimi sitaki ife ,"alisema Mkenda


"Ndani ya wiki hiyo moja nataka G32 iwe imeanza  kazi kwasababu Kazi ya ofisi ya Mrajisi inatakiwa iwe facilitative maana kuna wengine walikuwa wanazuia Kahawa isiende kwenye uchakataji ,"alisema Profesa Mkenda


Akizungumza mara baada ya waziri kutoa agizo hilo, Meneja Mradi wa G32, Gabriel Ulomi aliishukuru serikali kwa maamuzi hayo na kusema kuwa ni moja ya hatua ya kuwarejeshea uhai.


"Kwa niaba ya kundi la vyama vya G32 tunashukuru awamu ya sita kusikiliza kilio cha wakulima wa Kahawa ambao tumekuwa tukikusanya Kahawa kutoka kwa wakulima na kuuza ndani na nje ya nchi kwa kurejeshea haki yetu ya kimsingi ya kufanya biashara kwa sheria za nchi kwa sababu ushirika ni uhai,"alisema Ulomi


"Sisi tulikuwa tukilazishwa na Mrajisi kurudi kwenye ushirika ambao una matatizo ambayo matatizo haya yaliyotokea G32 ikaanza yalikuwa hayajarekebishwa, tunamshukuru Waziri amesikiliza  hilo na kuturudishia uhai wetu na hatutamwangusha ,"alisema Ulomi


MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com