METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 28, 2021

KUMBI ZA BURUDANI TOENI FURSA KWA BENDI ZA MUZIKI WA DANSI NA WASANII WACHANGA:NAIBU WAZIRI GEKUL

 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul ametoa wito kwa wawekezaji wa kumbi za burudani nchini kutoa fursa kwa bendi za muziki wa dansi na wasanii wachanga kufanya maonesho  katika kumbi hizo ili kukuza na kuendeleza  Sanaa  nchini.

Mhe. Gekul amesema hayo Juni 25, 2021 mjini Kahama wakati akifungua eneo la kisasa la burudani lenye hadhi ya Kimataifa la “The Magic 101”.

“Natoa rai kwa wasimamizi wa eneo hili kutoa fursa kwa bendi za muziki wa dansi hususani bendi kongwe pamoja na wasanii wachanga wa hapa Shinyanga na maeneo mengine ya nchi kufanya maonesho katika eneo hili ili waweze kuonesha vipaji vyao na kujiongezea kipato” amesema Mhe. Gekul.

Mhe.Gekul amesema pamoja na kutoa fursa kwa vijana kutumia ukumbi huo pia amewaasa kutunza na kulinda maadili ya Mtanzania pamoja na kuwalinda vijana wadogo,  amesema hategemei kuwakuta wanafunzi na watoto wenye umri chini ya miaka 18 katika eneo hilo. 

Aidha, Naibu Waziri amewapongeza wamiliki wa Magic 101 kwa uwekezaji walioufanya na kutoa ajira kwa vijana wakitanzania zaidi ya 60, na kuwasisitiza wamiliki hao kulipa kodi stahiki kwa Serikali ili kuendelea kuchochea maendeleo ya Taifa.

Eneo la burudani la “The Magic 101” limegharimu zaidi ya Shingili Milioni Mia Tano  linatoa huduma za maonesho ya Sanaa na burudani, bar, chakula, mabwawa ya kuogelea (swimming pool) pamoja na chumba maalum cha joto kijulikanacho kama sauna.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com