Baadhi wananchi wa Manispaa ya Iringa wakiwa wamevikimbia viti kwa kuepuka kulipa shilingi mia tano ambayo hapo awali haikuwepo na kuwapelekea kukaa katika eneo ambalo limekuwa likitumika kutupia takataka mbalimbali za wananchi wanaoitumia bustani hiyo
Hivi ndio ukifika katika bustani iliyopo katika manispaa ya Iringa utakutana na maneno hayo ya kulipia kiti endapo utataka kukaa kwenye viti vilivyopo katika bustani hiyo.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wamelalamikia tozo ya shilingi mia tano anayolipishwa mwananchi kukaa kwenye viti vilivyopo katika Bustani ya manispaa ya Iringa.
Wakizungumza na blog hii wananchi hao walisema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha uongozi wa manispaa kutoza fedha wananchi ya kukaa kwenye viti hivyo tofauti ilivyokuwa sehemu nyingine za wazi kama hizo zinazomilikiwa na UMMA.
Walisema kuwa ukitembea kwenye Bustani nyingine za UMMA kama hii huwezi kukuta mwananchi anachajiwa pesa yoyote ile hii ndio mara ya kwanza kuiona Iringa kwa kuwanyima haki wananchi wake.
Walisema kuwa karibia eneo kubwa la Bustani hiyo limewekwa viti na vimeandikwa kukaa shilingi mia tano ndio maana wanakimbilia kukaa maeneo ambayo sio masafi kama ilivyo maeneo yaliyowekwa hivyo viti.
Wananchi hao waliongeza kuwa wananchi wengi wamekaa sehemu ambazo sio safi kwa kuwa maeneo yote mazuri yaliyopo kwenye Bustani hiyo ya manispaa ya Iringa yamewekwa viti vingi ambavyo vinachajiwa hiyo pesa ya shilingi mia tano.
"Unajua mwandishi kuja hapa tu ni utalii tosha hiyo wanavyoweka tozo ya kukaa kwenye viti hivyo kunapunguza wananchi kujifunza kutalii na kutembelea Bustani hiyo"walisema wananchi hao
Walimaliza kwa kuomba uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa kutafuta vyanzo vingine vya mapato katika Bustani hiyo na kuwaacha wananchi waendelee kufurahia kutalii ndani ya Bustani hiyo.
"Kuja hapa katika hii Bustani kunaongeza hali ya wananchi kujifunza kuendelea kutalii katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa" walisema wananchi hao.
Akijibia malalamiko ya wananchi naibu Meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Mh Kenyatta Likotiko alisema kuwa swala hiyo lilipelekwa kwenye kamati husika na kubaini tozo hiyo ambayo ilotolewa maelezo kuwa ni tozo ya kusaidia fedha za kufanyia usafi.
Alisema kuwa kamati ilipisha swala hilo kwa kuwa waliangalia kwa upana wa maslai ya halmashauri na utanzani wa Bustani yenyewe.
Aliongeza kuwa kuna maeneo mengi ambayo wananchi wanaweza kukaa bila kulipishwa isipokuwa kwenye hivyo viti ambavyo tayari vimetolewa maelezo.
0 comments:
Post a Comment