Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Kilimo chini ya
mwamvuli wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bwana Gerald Kusaya akiendesha kikao cha sita leo tarehe 01 Julai, 2020 kwenye
ukumbi wa Landmark hotel, Mbezi Beacha, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald
Kusaya ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Kilimo akiwa pamoja na Mama
Jacqueline Maleko Mwenyekiti mwenza wakati wa kikao cha sita cha Kikundi Kazi
katika hotel ya Landmark, Mbezi Beach, Jijini Dar es Salaam leo Tarehe 01
Julai, 2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald
Kusaya ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Kilimo akiwa pamoja na Wajumbe
wa Kikundi Kazi cha Kilimo leo katika hotel ya Landmark, Mbezi Beach, Jijini
Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mwenyekiti Mwenza Mama Jacqueline Maleko na
kulia kwake ni Dkt. Godwill Wanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Biashara (Picha zote na Issa Sabuni – Wizara ya Kilimo).
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya ametoa wito kwa Wakulima wa Tanzania
kujiunga katika vikundi ili kuunganisha nguvu na kuja na miradi mikubwa ambayo
itakuwa rahisi kupata mikopo kutoka kwenye Taasisi za Fedha kama Benki ya
Kilimo (TADB).
Katibu
Mkuu ameyasema hayo leo tarehe 01/07/2020 wakati akifungua kikao cha sita cha
Kikundi Kazi cha Kilimo chini ya Baraza la Taifa la Biashara, kikao
kilichofanyika katika hotel ya Landmark Jijini Dar es Salaam.
Bwana
Kusaya amesema Tanzania ya Viwanda inajengwa na Wakulima wanaolima kwa tija; Jambo
hilo haliwezekani bila ya msaada wa Taasisi za Fedha.
“Bila
ya mikopo hakuna miradi mikubwa itakayofanikiwa. Niwaombe Wakulima wa mazao
yote na hasa Wakulima wanaolima mazao yenye thamani kubwa kama mboga, matunda
na maua kuwa ili kilimo kichangie kwenye uchumi wa viwanda kwa kuzalisha
malighafi kwa ajili ya viwanda vyetu ni vyema Wakulima wawe kwenye vikundi; Kwa
kufanya hivyo, mtachangia kwenye uchumi wa viwanda.
Aidha
Katibu Mkuu Gerald Kusaya ameongeza kuwa Wakulima wa mazao mengi ya biashara
hawajiunga katika vikundi na kuongeza kuwa fursa nyingi za masoko ya kilimo
zinapatikana kwa kuwa kwenye vikundi.
“Wakulima
itumie fursa ya kupata mikopo na uwezeshaji kwa kukaa kwenye vikundi kama Vyama
vya Ushirika lakini pia tumie fursa ya masoko ya mazao kwa njia ya mitandao
kama SOKO LA BIDHAA TANZANIA (TMX).
“Soko
la bidhaa ni mahali rasmi ambapo wanunuzi na wauzaji wa bidhaa hukutanishwa
pamoja ambapo wote ni wanachama au huwakilishwa na Wanachama. Sasa ili Wakulima
wauze bidhaa au mazao yao ni vizuri wakawa katika vikundi”. Amekaririwa Katibu
Mkuu.
Soko
la bidhaa limegawanyika katika maeneo makubwa matatu ambayo ni: - Soko la mauzo
ya papo kwa papo - (Spot Exchanges). Bidhaa huuzwa kwa bei ya papo kwa
papo. Uchukuaji na malipo ya bidhaa
hufanyika sio zaidi ya siku mbili baada ya mauzo.
Eneo
la pili ni soko la mauzo ya mkataba unaotekelezwa baadaye (Futures exchanges).
Bei ya bidhaa hukubaliwa siku hiyo hiyo kwa malipo na uchukuaji bidhaa
utakaofanyika baada ya kipindi fulani, kwa mfano baada ya siku 90. Huwezesha
kujikinga na athari za kubadilika kwa bei.
Na
tatu ni soko la mauzo ya mkataba wenye uchaguzi wa kutekelezwa (Options). Bei
ya bidhaa hukubaliwa leo kwa ada na sio lazima malipo na uchukuaji bidhaa
ukafanyika baada ya kipindi kilichokubaliwa.
Kijani kibichi ipande tunapenda tujue masoko yote
ReplyDelete