Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na waandishi
wa Habari alipotembelea Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama
Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es
Salaam ambapo tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa
atayafungua rasmi.
Waziri wa
Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya
Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade), Dkt.Ng’wanza Kamata (Mwenye miwani) na
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bi.Latifa Khamis (wa pili kulia)
alipotembelea Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba
yanayofanyika katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo
tarehe 03 Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Waziri wa
Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akipata maelezo kutoka kwa Afisa
wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), alipotembelea banda hilo katika Maonesho
ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika
uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03 Julai
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Waziri wa
Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akipata maelezo kutoka kwa Afisa
wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA),alipotembelea banda hilo katika
Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika
katika uwanja wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 03
Julai Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa atayafungua rasmi.
Serikali imewataka Wananchi kuendelea kupenda bidhaa
zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini kwani chanzo cha nchi kufikia uchumi
wa kati ni pamoja na wananchi wake kupendelea bidhaa ambazo wanazizalisha wao
kama wao, na mafanikio yametokana na juhudi za watanzania wote wakiongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya 44 ya
Biashara ya Kimataifa (sabasaba) yanayofanyika
katika Uiwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda
na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa amesema kuwa ili watanzania waweza
kusheherekea mafanikio endelevu ya kuingia nchi zenye kipato cha kati
wanatakiwa kuwa wa kwanza kutangaza bidhaa zao.
"Kupitia mafanikio tuliyoyapata rai yangu kwa
watanzania ni kupenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu ili mafanikio haya
ya nchi kuwa kwenye orodha ya nchi zenye kipato cha kati yawe ni matunda kwa
watanzania hasa kwa wakina mama na
vijana wanaotafuta ajira na tukiendelea kupenda bidhaa zinazozalishwa
hapa nchini ndivyo tunazidi kutengeneza fursa za ajira kwa watanzania".
Alisema Mhe.Bashungwa.
alisisitiza kuwa watanzania wanatakiwa kuangalia bidhaa za
ndani Kabla hawajanunua bidhaa kutoka nje ili kuweza kukuza viwanda na kuwa na
uchumi wenye kipato cha kati endelevu kwani ili Watanzania waendelea
kusheherekea mafanikio haya ya kufikia kipato cha kati tunatakiwa kupenda
bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
Alibainisha kuwa kupitia maonesho 44 ya Biashara kimataifa
(sabasaba) ambapo takribani kampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi
zitashiriki, kutakuwa na fursa ya wananchi kuja kununua bidhaa na kuangalia
teknolojia mbalimbali zikioneshwa na taasisi na makampuni ya kitanzania, pia kupitia B2B wale ambao wapo nje
wataendelea kuingia mikataba na wafanyabiashara ambao wanashiriki katika
maonesho ya sabasaba hayo.
Pamoja na hayo Mhe. Bashungwa amesema Tanzania kuwa nchi
yenye kipato cha kati inasaidia kuingia kwenye rada ya kimataifa hivyo wengi
watapenda kuja kuwekeza hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment