Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Bwana Gerald Kusaya akiongea na Wadau wa zao la Chai pamoja na
Wazalishaji wa mbolea mapema leo tarehe 02/07/2020 katika Ofisi za Mamlaka ya Udhibiti
wa Mbolea (TFRA) kulia kwa Katibu Mkuu ni Dkt. Stephan Ngailo, Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini
Sehemu
ya Wadau wa mkutano huo wakiendelea na majadiliano kuhusu maendeleo ya tasnia
ya mbolea pamoja na zao la chai
Sehemu ya Wadau wa mkutano
huo kutoka Idara ya Maendeleo ya Mazao, Wizara ya Kilimo, Taasisi ya Utafiti wa
Kilimo (TARI), Bodi ya Chai Tanzania (TBT), Wakala wa Maendeleo ya Wakulima
Wadogo wa Chai (TASHTIDA), Taasisi ya Utafiti wa zao la Chai Tanzania (TRIT), Kampuni
ya Minjingu Mines and Fertilizer Ltd (MMFL), UNILIVER TANZANIA LTD pamoja na Wawakilishi
kutoka Vyama vya Ushirika vya Chai Tanzania - (AMCOS za Chai) na Menejimenti ya
TFRA wakimsikiliza Katibu Mkuu Kilimo Bwana Gerald Kusaya alipokwa akiongelea
mambo mbalimbali yanayohusiana na tasni ya mbolea nchini
Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Bwana Gerald Musabila Kusaya kusaya amesema Tanzania ina nafasi yakubwa
ya kuleta mapinduzi makubwa katika Sekta ya Kilimo ikiwa kila Mdau kwenye
mnyororo wa thamani atatimiza wajibu wake ipasavyo.
Katibu Mkuu Kusaya
ameyasema hayo, leo tarehe 02/07/2020 wakati wa kikao maalum alichokiitisha ili
kujadiliana na Wadau wa zao la chai pamoja na Wazalishaji wa mbolea maalum ya zao
la chai; Inayoitwa Minjingu Chai katika Ukumbi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea
(TFRA) Jengo la Kilimo I, Jijini, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kusaya amesema
Mkulima anategemea maendeleo ya utafiti kwenye tasnia ya mbolea, anategemea
ushauri mzuri wa Maafisa Ugani, anategemea kwa sehemu kubwa uzalishaji wa
mbolea ambao utamuakikishia kupatikana kwa wakati na kwa bei nafuu lakini pia
Mkulima anategemea Ushirika imara ili awe na uhakika wa kuuza mazao yake baada
ya kuvuna.
Bwana Gerald Kusaya
ameongeza kuwa pembejeo moja ya muhimu katika ukuaji wa Sekta ya Kilimo ni
mbolea na kwamba mazingira ya Tanzania yanatoa fursa nyingi kwa viwanda vingi
kuanzishwa licha ya kukiri kuwa kuna changamoto kadhaa ambazo Serikali imekuwa
ikiendelea kuzitatua ili siku moja mazingira ya uwekezaji yawe mazuri kwa
kiwangi kikubwa.
Bwana Gerald Kusaya
ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuweka jitihada na kuweka mazingira mazuri
na wezeshi katika uwekezaji na ujenzi wa viwanda vya mbolea nchini. Aidha,
sambamba na jitihada hizo, pia kuna fursa mbalimbali zinazohamasisha uwekezaji
katika shughuli za uzalishaji wa mbolea nchini.
Amezitaja fursa hizo kuwa
ni pamoja na: - Uwepo wa utashi wa kisiasa unaoruhusu uwekezaji katika tasnia
ya mbolea.
“Tanzania ni kitovu cha
usambazaji katika mataifa ya Jumuia ya Afica ‘SADC’ ambayo hayana bandari.
Uwepo wa Wahandisi wa Kemikali “Chemical Engineers” wenye taaluma ya kuzalisha
mbolea wa kutosha katika soko la ajira.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.
Bwana Gerald Kusaya ametaja
fursa nyingine ni pamoja na uwepo wa Vituo vya Utafiti wa mazao ya kilimo; Yanayotumia
mbolea. Uwepo na nia ya makampuni binafsi yanayojihusisha na uwekezaji wa mbolea
na visaidizi vyake. Kufunguliwa kwa mipaka ya kuuza mazao nje ya nchi
inayohamasisha kuwepo kwa mahitaji makubwa ya mbolea na visaidizi vyake.
Katibu Mkuu Kusaya ameongeza
kuwa kuwepo kwa soko kubwa la ndani na nje la mahitaji ya mbolea na visaidizi
vyake. Uwepo wa Miundombinu kama nishati na barabara inayowezesha usafirishaji
wa mbolea kutoka bandarini hadi kwa mkulima wa mwisho.
Uwepo wa malighafi za
kuendeshea viwanda zinazotokana na mazao ya kilimo ambayo yanazalishwa kwa
kutumia mbolea pamoja na uwepo wa viwanda vingi vinavyotumia malighafi za mazao
ya kilimo; hivyo kufanya mahitaji ya mbolea kuongezeka.
Aidha Katibu Mkuu Bwana
Gerald Kusaya amekiri kuwa tasnia ya mbolea inakabiliwa na changamoto kadhaa
ikiwemo; Gharama kubwa za uwekezaji na uzalishaji zinazofanya mbolea
zinazozalishwa nchini kuwa na bei kubwa kuliko zinazoingia nchini.
Ameongeza kuwa kuwepo na
mifumo ya kisheria yenye utata ambayo inamlazimisha mwekezaji kushughulikia
masuala mengine ambayo yanaweza kufanywa na taasisi zingine.
Pamoja na kukosekana kwa
ushirikiano “collaboration” na watengenezaji wa bidhaa saidizi kama kutengeneza
vifungashio, kuweka maandishi kwenye mifuko.
“Changamoto tajwa hapo juu
zinaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuundwa kwa jopo la kiwizara ili kuimarisha
mahusiano na Ofisi ya Rais TAMISEMI na kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya
Mbolea Namba 9 ya Mwaka 2009 kuhusu usimamizi wa uwekezaji katika viwanda vya
mbolea (Interministerial Commitee).” Amekaririwa Bwana Gerald Kusaya.
Katibu Mkuu Kusaya amesema Bodi
ya TFRA inajukumu la kuboresha mazingira ya uwekezaji katika viwanda na
kurekebisha sheria ya mbolea na miongozo inayohamasisha Wawekezaji waliopo
kuzalisha kulingana na uwezo wa kiwanda.
“TFRA iendelee kusimamia na
kuhakikisha kwamba viwanda vyote vya mbolea na visaidizi vyake nchini
vinasajiliwa na kuwa na leseni hai muda wote.”
“TFRA iendelea kufuatilia
na kutoa ushauri kwa wawekezaji wa viwanda vya mbolea kukamilisha nyaraka zote
muhimu zinazotakiwa ili waweze kukidhi vigezo vya kuanzisha viwanda vya
mbolea.”
“TFRA iendelee kushirikiana
na Taasisi za utafiti na wadau wengine wa maendeleo katika kuelimisha umma juu
ya umuhimu wa matumizi sahihi y mbolea.”
“TFRA iendelee kuhamasisha
wadau mbalimbali wa kilimo kupitia vyombo vya habari na maonesho ya kilimo ili
wawekeze katika tasnia ya mbolea.” Amekaririwa Katibu Mkuu akitoa maagizo hayo
kwa Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Mbolea nchini (TFRA).
Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Bwana Gerald Kusaya yupo Jijini Dar es Salaam, ambapo tangu siku ya
Jumanne tarehe 30 Juni, 2020 hadi Ijumaa tarehe 03 Julai, 2020 atakuwa
akizitembela Taasisi za Wizara ya Kilimo, zilizopo Jijini, Dar es Salaama na
baadae anataraji kuanza ziara ya kutembelea ili kujionea changamoto na maendeleo
ya Sekta ya Kilimo mazao katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ziara ambayo
inataraji kuanza tarehe 08 Julai, 2020.
0 comments:
Post a Comment