Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge ,akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakati wa kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo katika hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Gerald Kusaya,akizungumza kabla ya kuingia Makubaliano ya Mkataba na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo katika hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Utawala JKT ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi JKT Kanali Hassan Mabena,akitoa taarifa kabla ya kusainiwa mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo na Wizara ya Kilimo katika hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakitiliana sahihi ya Mkataba wa ushirikiano wa kuboresha sekta ya kilimo hafla iliyofanyika leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT, yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakibadilisha hati mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakionyesha hati ya mkataba mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) akimkabidhi zawadi ya saa ya ukutani Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya akionyesha zawadi yake aliyokabidhiwa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),Meja Jenerali Charles Mbunge mara baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT,yaliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Wizara ya Kilimo na
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)zimetiliana saini mkataba wa makubaliano ya
ushirikiano katika sekta ya kilimo ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya
Tano katika kuzalisha kwa tija ili kuiliwezesha Taifa kuwa na ziada ya chakula
na mazao ya biashara.
Hayo yamesemwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald
Kusaya leo Februari 26, 2021
makao makuu ya JKT wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kutiliana
saini mkataba huo kati ya Wizara hiyo na JKT kwa lengo la kuimarisha zaidi ushirikiano
uliopo kati ya pande hizo.
“Makubaliano haya ni
ya miaka mitano na baadhi ya maeneo ya ushirikiano ni pamoja na; kuimarisha
teknolojia bora za uzalishaji zinazoendana na wakati,Kujenga uwezo wa kusambaza
teknolojia za kilimo, Huduma za umwagiliaji, Utafutaji masoko, huduma za
usimamizi wa mazao ikiwemo kuongeza thamani mazao ikiwemo mpunga utakaozalishwa
kupitia kikosi cha Chita Kilombero mkoani Morogoro”, alisisitiza Kusaya.
Akifafanua Bw. Kusaya
amesema kuwa makubaliano hayo
yatawezesha Wizara ya Kilimo na JKT kufanya tafiti za pamoja,kuanzisha mpango
wa pamoja wa usambazaji wa taarifa za kilimo ikiwemo teknolojia,kubadilishana
taarifa za masoko, kufanya usimamizi na tathmini ya pamoja.
Kwa upande wake Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali
Charles Mbuge amepongeza
ushirikiano uliopo kati ya JKT na Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi zilizopo
chini ya Wizara hiyo ikiwemo Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI).
Aidha, Meja Jenerali
Mbuge ameleza kuwa Jeshi hilo ni chombo pekee ambacho kikitumika katika kukuza sekta ya kilimo kitaleta
matokeo makubwa katika sekta ya kilimo ambapo aliahidi kuendelea kushirikiana
na Wizara ya Kilimo ili kuhakikisha kuwa malengo yaliyopangwa yanafikiwa.
“ JKT katika mwaka
2019/ 2020 na 2020/2021 imeanzisha kilimo cha kimkakati katika maeneo
mbalimbali ikiwemo kupitia kikosi cha Chita wilayani Kilombero mkoani Morogoro ambapo inazalisha mpunga kwenye eneo
la ekari 2500 na baadae ekari 12,500 ambapo lengo ni kuongeza uzalishaji mara
mbili zaidi.
Aliongeza kuwa JKT
inatumaini kuwa Wizara ya Kilimo itasaidia katika kuwezesha ujenzi wa maghala
katika vikosi vya Jeshi hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Tawi la Utawala JKT ambaye pia
Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
JKT Kanali Hassan Mabena amesema kuwa wamechukua hatua za makusudi
katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili kutimiza azma ya Taifa
kujitegemea kwa chakula na pia kuzalisha mazao ya biashara.
Aidha, Kanali Mabena
amesema kuwa JKT imekuwa na ushirikiano mzuri na TARI, ASA na Taasisi nyingine
zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo.
Aliongeza kuwa katika
kuimarisha uzalishaji JKT imenunua matrekta 15 pamoja na zana nyingine za
kilimo kwa lengo la kuzalisha kwa tija.
Makubaliano kati ya JKT na Wizara ya Kilimo yanatajwa kuwa chachu ya ukuaji wa sekta hiyo hapa nchini na kuwezesha Taifa kujitegemea na kuuza ziada itakayozalishwa.
0 comments:
Post a Comment