METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, February 27, 2021

Rais Magufuli amuapisha Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Balozi kabla ya kumuapisha tena kuwa Katibu Mkuu Kiongozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Februari 2021. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Februari 2021.  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Kamishna wa Maadili Jaji wa Mahakama ya Rufani, Sivangilwa Sikalaliwa Mwangesi kushoto alipokuwa akiongoza Kiapo cha Maadili kwa Viongozi wa Umma kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Februari 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com