Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akihutubia Wadau wa Mkutano wa Kikanda wa Uwekezaji na Biashara ya Mazao ya Bustani katika ukumbi wa Hoteli ya Hayatt Regency ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akihutubia Wadau wa Mkutano huo wa Kikanda wa Uwekezaji na Biashara ya Mazao ya Bustani katika ukumbi wa Hoteli ya Hayatt Regency ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Abubakar Kunenge.
Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Bwana Gerald Kusaya leo mchana tarehe 5 Disemba 2020 amemuahidi Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) pamoja na Wadau
wa Sekta ya Kilimo cha mazao ya bustani kuwa Wizara ya Kilimo itaendelea
kushirikiana na Wizara nyingine kama Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Balozi za
Tanzania nje ya nchi katika kutafuta masoko ya mazao ya bustani (Mbogamboga,
matunda, maua na viungo) ili kuongeza akiba ya fedha za kigeni nchini.
Katibu Mkuu Kilimo
Bwana Gerald Kusaya ameyasema hayo wakati akiwahutubia Wadau wa Mkutano wa
Kikanda wa Mazao ya bustani; Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Hayatt
Regency ambapo Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Asasi ya Mazao ya Bustani
(TAHA) zilianda mkutano huo wa siku moja.
Katibu Mkuu Kilimo
Bwana Gerald Kusaya ameongeza kuwa mwaka 2019 Serikali kupitia Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilifanya utafiti wa masoko katika
nchi za Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Nchi za Kiarabu ambapo kupitia
Ushirikiano huo, Tanzania iliuza mazao kwenye nchi hizo.
Pamoja na mazao ya
bustani kuuzwa katika nchi ya Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Farme za Kiarabu;
Jumla ya dola milioni 779 za Marekani zilipatikana kutokana na uuzwaji kuuza
mazao hayo duniani kote.
“Tayari, zaidi ya tani
150 za parachichi, mananasi na pilipili kali zimekwishauzwa kwenye hayo masoko
jambo ambalo ni matokeo makubwa ya namna ambavyo Serikali inaweza kufanya kazi
na sekta binafsi na kuleta matokeo makubwa chanya.” Amekaririwa Katibu Mkuu
Kusaya.
Katibu Mkuu Kusaya
ameongeza kuwa suala la kutafuta masoko ya uhakika ni mkakati wa kitaifa.
“Ili kuweza kuyafanyia
kazi kwa mapana yake masuala ya upatikanaji wa masoko, Wadau wa Sekta ya
Kilimo, kupitia Kamati ya Ufundi yenye wawakilishi toka taasisi mbalimbali za
Serikali na Binafsi imeanza kuandaa Mkakati wa Masoko ya mazao ya bustani au
kwa kiingereza Horticulture Industry Market Access Strategy – HIMAS). Mkakati
huo utaainisha maeneo muhimu ya kufanyiwa kazi ili kuboresha upatikanaji wa
masoko na kutukwamua toka hapa tulipo.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.
Katibu Kusaya
ameongeza kuwa ili kuimaisha usimamizi wa masuala ya afya ya mimea na
viuatilifu, mwezi Juni mwaka 2020 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
lilipitisha Sheria mpya ya Afya ya Mimea ambayo pamoja na mambo mengine
inaanzisha Mamlaka ya Afya ya Mimea na Udhibiti wa Viuatilifu na kuongeza kuwa
hatua hiyo imelenga kuimarisha usimamizi na huduma kwa kuwa na Mamlaka moja
itakayosimamia shughuli zilizokuwa zilizokuwa zinafanywa na TPRI na Kitengo cha
Afya ya Mimea cha Wizara ya Kilimo; Ambapo kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo
kutaongeza ubora wa mazao yakiwemo, mazao ya horticulture kwa ajili ya masoko
ya ndani na nje ya nchi.
Kwa kuongezea Katibu
Mkuu Kusaya amesema Wizara ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itaendelea
kushirikiana na Wadau kuzipatia ufumbuzi changamoto katika Sekta ya kilimo ili
Sekta iendelee kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi, ajira na
upatikanaji wa malighafi za viwanda ambapo takribani asilimia 5 za makighafi za
viwanda zinategemea kilimo.
Aidha Katibu Mkuu
Kilimo Bwana Gerald Kusaya ameipongeza Asasi ya TAHA inayoongozwa Dkt.
Jacqueline Mkindi kwa kufanikisha mkutano huo na kuongeza kuwa Yeye kama
Mtendaji Mkuu ataendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa tasnia ya
mazao ya bustani inasonga mbele.
“Niseme kwamba jitihada hizi za Wizara kwa kushikiana na Sekta Binafsi chini ya uratibu wa TAHA; Zote zinalenga kuifanya nchi yetu kuwa mhimili wa uzalishaji na usambazaji wa mazao ya horticulture na mazao mengine kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi. Masoko ya Kikanda, yanaonekana kuwa fursa kubwa kwa kilimo chetu cha mazao ya bustani (horticulture) na leo hii tunakutana ili kutafuta namna ambavyo nchi yetu inaweza kufaidika nayo. Wizara ya kilimo itaendelea kuratibu shughuli za kuimarisha Sekta hii na kuhakikisha kuwa Wakulima wanafaidika nayo.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.
0 comments:
Post a Comment