METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, November 18, 2020

WANANCHI WA IRINGA WAMETAKIWA KUENDELEA KUJIKINGA NA MAGONJWA MILIPUKO

Mkuu wa wilaya ya Iringa alipokuwa akihamasisha wananchi kujinga na virusi vya Corona hasa kwenye usafiri wa UMMA (PICHA KUTOKA MAKTABA)

Na Fredy Mgunda,Iringa

Licha ya serikali kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga na maaambukizi ya virusi vya corona bado baadhi ya wananchi manispaa ya iringa wamekuwa wakipuuza zoezi hilo.

 

Wakizungumza na vyog hii baadhi ya wananchi hao walisema kuwa jamii imekuwa ikipuuza uvaaji sahihi wa vifaa vya kujikinga na corona   ikiwemo kuvaa barakoa kwa siku tatu bila kuifua jambo linaloweza kuhatarisha maambukizi mapya.

 

Wananchi hao walisema kuwa wanapaswa kuendelea kutumia vizuri vifaa hivyo vya kujikinga dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona ili kuweza kuweka jamii katika sehemu salama zaidi.

 

"Wananchi wengi saizi wameacha kunawa mikono au kutakasa mikono yao Kutokana na kuamini kuwa ugonjwa huo umeisha jambo ambalo sio sahihi kutokana na Corona kuwepo kwenye nchi jirani jambo ambalo linasisitizwa na serikali kuendelea kujinga na Corona"walisema

 

Baadhi ya wananchi hao aliongeza kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakivaa barakoa zaidi ya masaa matatu au wakizaa barakoa hizo tofauti na mashariti sahihi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Corona 

 

 Rose Bilas ni mdau wa masuala ya Afya  mkoani Iringa alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kusikiliza vyombo mbalimbali vya habari ili kujua nini kinaendelea na kupata elimu ya virusi vya Corona kutoka katika taasisi za kiserikali na taasisi nyingine. 

 

Naye Richard Kiza mdau wa masuala ya Afya mkoa Iringa  aliishauri jamii kuendelea kufuata ushauri uliowekwa na wataalamu wa afya ikiwemo kutumia barakoa kwa usahihi pamoja na kutumia vitakasa mikono ili kujikinga na corona.

 

 Kwa upande wake Afisa Mradi wa boresha afya kupitia shirika la IDYDC mkoani Iringa Casto David alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi ya kujikinga na Corona huku akiwataka wananchi kuendelea kuzingatia usafi.

 

Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea kuzingatia kufanya usafi na kuwa wasafi muda wote ndio njia sahihi kuepukana na maambukizi ya virusi vya Corona hapa nchini hususan mkoa wa Iringa. 

 

David alisema wamekua wakitoa elimu mara kwa mara kwa viongozi mbalimbali juu ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona hasa katika yote ya umma 

 

Serikali kupitia Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto imesema kuwa ili kukabiliana na maambukizi ya Corona ni vyema wananchi wakaepukana na mikusanyiko isiyokuwa na lazima, kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji Tiririka na sabuni pamoja na kutumia vitakasa mikono.

 

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com