Licha ya serikali kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga na maaambukizi ya virusi vya corona bado baadhi ya wananchi manispaa ya iringa wamekuwa wakipuuza zoezi hilo.
Wakizungumza
na vyog hii baadhi ya wananchi hao walisema kuwa jamii imekuwa ikipuuza uvaaji
sahihi wa vifaa vya kujikinga na corona ikiwemo kuvaa barakoa kwa
siku tatu bila kuifua jambo linaloweza kuhatarisha maambukizi mapya.
Wananchi
hao walisema kuwa wanapaswa kuendelea kutumia vizuri vifaa hivyo vya kujikinga
dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona ili kuweza kuweka jamii katika sehemu
salama zaidi.
"Wananchi
wengi saizi wameacha kunawa mikono au kutakasa mikono yao Kutokana na kuamini
kuwa ugonjwa huo umeisha jambo ambalo sio sahihi kutokana na Corona kuwepo
kwenye nchi jirani jambo ambalo linasisitizwa na serikali kuendelea kujinga na
Corona"walisema
Baadhi
ya wananchi hao aliongeza kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakivaa barakoa
zaidi ya masaa matatu au wakizaa barakoa hizo tofauti na mashariti sahihi ya
kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Corona
Rose
Bilas ni mdau wa masuala ya Afya mkoani Iringa alisema kuwa wananchi
wanapaswa kuendelea kusikiliza vyombo mbalimbali vya habari ili kujua nini
kinaendelea na kupata elimu ya virusi vya Corona kutoka katika taasisi za
kiserikali na taasisi nyingine.
Naye Richard
Kiza mdau wa masuala ya Afya mkoa Iringa aliishauri jamii kuendelea
kufuata ushauri uliowekwa na wataalamu wa afya ikiwemo kutumia barakoa kwa
usahihi pamoja na kutumia vitakasa mikono ili kujikinga na corona.
Kwa
upande wake Afisa Mradi wa boresha afya kupitia shirika la IDYDC mkoani Iringa
Casto David alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi ya kujikinga na
Corona huku akiwataka wananchi kuendelea kuzingatia usafi.
Alisema
kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea kuzingatia kufanya usafi na kuwa wasafi muda
wote ndio njia sahihi kuepukana na maambukizi ya virusi vya Corona hapa nchini
hususan mkoa wa Iringa.
David alisema wamekua wakitoa elimu mara kwa mara kwa viongozi mbalimbali juu ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona hasa katika yote ya umma
Serikali
kupitia Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto imesema kuwa
ili kukabiliana na maambukizi ya Corona ni vyema wananchi wakaepukana na
mikusanyiko isiyokuwa na lazima, kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji Tiririka
na sabuni pamoja na kutumia vitakasa mikono.
MWISHO
No comments:
Post a Comment