Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini Hamid Njovu amemtangaza mgombea wa udiwani wa kata ya Igumbilo kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Boniface kilave amepita bila kupingwaWaandishi wa habari wakimsikiliza Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini Hamid Njovu akimtangaza mgombea wa udiwani wa kata ya Igumbilo kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Boniface kilave amepita bila kupingwa
Na Fredy Mgunda,IringaMSIMAMIZI wa uchaguzi wa jimbo
la Iringa Mjini Hamid Njovu amemtangaza mgombea wa udiwani wa kata ya Igumbilo kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Boniface kilave amepita bila kupingwa baada ya
wagombea wa vyama vingine kujiondoa kugombea udiwani kwenye kata hiyo.
Akitangaza maamuzi hayo
msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini Hamid Njovu, alisema kuwa
wagombea wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Wilbert Kilave na
mgombea wa chama cha ACT WAZALENDO, Mahamad Rassa walimwandikia barua za
kujiondoa kwenye uchaguzi huo huku wakiwa wameambanisha na viapo vya tamko la
kujitoa vilivyotolewa mbele ya hakimu mnamo tarehe 17/11/2020
Alisema kuwa barua hizo za
kujiondoa zilizingatia kifungu cha 50 cha sheria ya uchaguzi wa serikali za
mitaa (uchaguzi wa madiwani) Sura ya 292 ya mwaka 2015 na kanuni zake.
Njovu aliongeza kuwa mgombea
huyo wa udiwani aliyepita bila kupigwa atakabidhiwa hati ya kuchaguliwa kuwa
diwani ya kata hiyo ya Igumbilo tarehe 8/12/2020 siku ambayo uchaguzi ulitakiwa
kufanyika.
Aidha Msimamizi huyo wa
uchaguzi alitangaza kuwa jimbo la Iringa Mjini litakuwa na madiwani wa chama
kimoja ambacho ni chama cha mapinduzi (CCM) pekee
Uchaguzi huo ulitakiwa
kufanyika kutokana na kifo kilichotokea cha tarehe 16/10/2020 na kumpa mamlaka ya kuitisha uchaguzi upya
kwa mujibu wa kanuni ya 33(1) na (2) ya kanuni ya uchaguzi wa uchuguzi wa
serikali za mitaa (uchaguzi wa madiwani),sura ya 292 ambazo zilipelekea msimamizi
wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini
kutoa taarifa tume ya taifa uchaguzi kuhusu kifo cha mgombea udiwani wa chama
cha mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment