Wananchi wa halmashauri ya manispaa ya iringa wamewashauri wamiliki wa taasisi binafsi na serikali kuendelea kuweka vifaa vya kujikinga na virusi vya corona(covid 19 ) ili kujikinga na kuwakinga wengine na maambukizi ya homa kali ya mapafu.
Wakizungumza na blog hii wananchi
hao walisema kuwa wadau wa serikali na binafsi waendelee kutoa elimu juu ya
umuhimu wa kujikinga na covid 19 wasisubiri uzuke ndio waanze kuchukua
tahadhari ya kutoa elimu.
Wananchi
hao walisema kuwa wanatakiwa kuendelea kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa
Corona kutoka na ugonjwa huo ukiwa bado unaendelea kusambaa kwenye nchi
nyingine kama vile majirani zetu.
Walisema
kuwa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya milipuko vinatakiwa
kuendelea kutumiwa kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya milipuko kama vile
ambavyo ugonjwa wa Corona ulivyokuja kwa kasi hapa nchi.
"Tanzania
bado inafanya biashara na mwingiliano na wananchi wa mataifa mengine wanaongia
nchini kutoka kwenye mataifa ambayo bado yanaugonjwa wa Corona hivyo serikali
na taasisi mbalimbali ziendelee kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya
ugonjwa wa Corona"walisema
Naye mratibu wa afya wa
halmashauri ya manispaa ya iringa Theopist Kwintini alisema manispaa
wameweka mikakati ya kuendelea kuhamasisha jamii na taasisi mbalimbali
kuendelea kujikinga na ugonjwa wa corona mpaka wizara itakapotangaza
rasim kuwa ugonjwa huo umetoweka hapa nchini.
Alisema kuwa wamekuwa wakitoa
elimu mara kwa mara kwa njia mbalimbali kama vile mikutano ya hadhara na vyombo
vya habari ili kuendelea kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Corona ambao bado
haujaisha kabisa.
Kwintini
alisema kuwa ugonjwa wa Corona bado upo hivyo taratibu zote za kujikinga dhidi
ya ugonjwa huo zinapaswa kuendelea kufuatwa kama ilivyokuwa hapo awali ili
kuendelea kuilinda jamii ya watanzania na dunia kwa ujumla.
"Juzi
hapa nilitembelea benki ya NMB tawi la Mkwawa wao bado wanachukua tahadhari
zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya covid19 kwa lengo la kuwalinda
wateja wao ambao wanapata huduma kwenye benki hiyo"alisema
Kwintini
alisisitiza kuwa taasisi zote za serikali na taasisi mbalimbali binafsi
wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona na kuendelea kutoa
elimu kwa wananchi wanaowaongoza.
Kwa upande wake Mganga Mkuu
Mkoa wa Iringa Dr. ROBERT SALIMU amewashauri wamiliki wa taasisi binafsi na
vyombo vya usafiri kuendelea kuchukua taadhari juu ya kujikinga na maambukizi
virusi vya corona pamoja na kula mboga za majani kwa wingi.
Alisema kuwa wamiliki wa
vyombo vya usafiri wanatakiwa kuendelea kuchua tahadhari ya kujikinga dhidi ya
ugonjwa wa Corona ili kuepusha madhara mengine yanayoweza kutokea kutokana na
ugonjwa huo ambao bado haujaisha kabisa hivyo tahadhari ni bora kuliko
tiba.
"Kwenye usafiri wa umma bado
abiria wanaendelea kujazana sana bila kujali tahadhari yeyote ile ya kujikinga
dhidi ya ya ugonjwa wa Corona kwa wananchi wote wanatumia usafiri huo kwa kuwa
ugonjwa huo bado haujapata dawa maalumu" alisema
Hata hivyo sekali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kama ilivyo nchi nyingine duniani zikiwemo za Africa Mashariki ipo katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu ambao umeingia nchini tangu tarehe 16 march 2020 ambapo Rais wa Tanzania dK John Magufuli aliutangazia umma kuwa ugonjwa huo umeendelea kutoweka.
0 comments:
Post a Comment