Tuesday, November 17, 2020

TAASISI ZA SERIKALI NA BINAFSI ZASHAURIWA KUENDELEA KUWEKA VIFAA VYA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA (COVID 19 )

Mkurugenzi wa kampuni ya Qwihaya General Enterprises Leonard Mahenda (kushoto) akimkabidhi msaada wa vifaa vya kujikinga na Corona, mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ( picha kutoka maktaba)


Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

Wananchi wa halmashauri ya manispaa ya iringa  wamewashauri wamiliki wa taasisi binafsi na serikali kuendelea kuweka vifaa vya kujikinga na virusi vya corona(covid 19 ) ili kujikinga na kuwakinga wengine na maambukizi ya homa kali  ya mapafu. 

 

Wakizungumza na blog hii wananchi hao walisema kuwa wadau wa serikali na binafsi waendelee kutoa elimu juu ya umuhimu wa kujikinga na covid 19 wasisubiri uzuke ndio waanze kuchukua tahadhari ya kutoa elimu.

 

Wananchi hao walisema kuwa wanatakiwa kuendelea kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kutoka na ugonjwa huo ukiwa bado unaendelea kusambaa kwenye nchi nyingine kama vile majirani zetu. 

 

Walisema kuwa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya milipuko vinatakiwa kuendelea kutumiwa kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya milipuko kama vile ambavyo ugonjwa wa Corona ulivyokuja kwa kasi hapa nchi. 

 

"Tanzania bado inafanya biashara na mwingiliano na wananchi wa mataifa mengine wanaongia nchini kutoka kwenye mataifa ambayo bado yanaugonjwa wa Corona hivyo serikali na taasisi mbalimbali ziendelee kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona"walisema 

 

Naye mratibu wa afya wa halmashauri ya manispaa ya iringa Theopist Kwintini alisema manispaa wameweka mikakati ya kuendelea kuhamasisha jamii  na taasisi mbalimbali kuendelea kujikinga  na ugonjwa wa corona mpaka wizara itakapotangaza rasim kuwa ugonjwa huo umetoweka hapa nchini.

 

Alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara kwa njia mbalimbali kama vile mikutano ya hadhara na vyombo vya habari ili kuendelea kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Corona ambao bado haujaisha kabisa. 

 

Kwintini alisema kuwa ugonjwa wa Corona bado upo hivyo taratibu zote za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo zinapaswa kuendelea kufuatwa kama ilivyokuwa hapo awali ili kuendelea kuilinda jamii ya watanzania na dunia kwa ujumla.

 

"Juzi hapa nilitembelea benki ya NMB tawi la Mkwawa wao bado wanachukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya covid19 kwa lengo la kuwalinda wateja wao ambao wanapata huduma kwenye benki hiyo"alisema

 

Kwintini alisisitiza kuwa taasisi zote za serikali na taasisi mbalimbali binafsi wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaowaongoza. 

 

Kwa upande wake Mganga Mkuu Mkoa wa Iringa Dr. ROBERT SALIMU amewashauri wamiliki wa taasisi binafsi na vyombo vya usafiri kuendelea kuchukua taadhari juu ya kujikinga na maambukizi virusi vya corona pamoja na kula mboga za majani kwa wingi.

 

 Alisema kuwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wanatakiwa kuendelea kuchua tahadhari ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Corona ili kuepusha madhara mengine yanayoweza kutokea kutokana na ugonjwa huo ambao bado haujaisha kabisa hivyo tahadhari ni bora kuliko tiba. 

 

"Kwenye usafiri wa umma bado abiria wanaendelea kujazana sana bila kujali tahadhari yeyote ile ya kujikinga dhidi ya ya ugonjwa wa Corona kwa wananchi wote wanatumia usafiri huo kwa kuwa ugonjwa huo bado haujapata dawa maalumu" alisema 

 

 Hata hivyo sekali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kama ilivyo nchi nyingine duniani zikiwemo za Africa Mashariki ipo katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu ambao umeingia nchini tangu tarehe 16 march 2020 ambapo Rais wa Tanzania dK John Magufuli aliutangazia umma kuwa ugonjwa huo umeendelea kutoweka.

No comments:

Post a Comment