Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga Wa pili kushoto) wakizungumza na Balozi wa Norway nchini, Elisabeth Jacobsen (wa pili kulia) baada ya Waziri mkuu kuzindua rasmi programu ya ugawaji wa mbolea kwa wakulima katika ofisi za Kampuni ya YARA Tanzania jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2020. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya YARA Tanzania, Winstone Odhiambo na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akinyanyua bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa programu ya ugawaji wa mbolea kwa wakulima katika ofisi za Kampuni ya YARA Tanzania jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa programu ya ugawaji wa mbolea kwa wakulima katika ofisi za Kampuni ya YARA Tanzania iliyofanyika Mtaa wa Kurasini jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa programu ya ugawaji wa mbolea kwa wakulima katika ofisi za Kampuni ya YARA Tanzania iliyofanyika Mtaa wa Kurasini jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2020.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akitoa maelezo ya awali wakati wa uzinduzi rasmi wa programu ya ugawaji wa mbolea kwa wakulima katika ofisi za Kampuni ya YARA Tanzania iliyofanyika Mtaa wa Kurasini jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa programu ya ugawaji wa mbolea kwa wakulima katika ofisi za Kampuni ya YARA Tanzania iliyofanyika Mtaa wa Kurasini jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Tarehe 11 Octoba 2020 amezindua Programu ya Action Africa ya ugawaji wa mbolea ya bure aina ya NPK kwa wakulima nchini inayotolewa na kampuni ya YARA.
Mbolea hiyo yenye gharama ya shilingi Bilioni 16.5 itasambazwa kwa wakulima 83,000 kote nchini watakaojiandikisha kwa njia ya simu ya kiganjani.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika mtaa wa Kurasini Jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa inasimamia kwa weledi utekelezaji wa ugawaji wa mbolea hiyo ili iweze kuwafikia wakulima kama ilivyokusudiwa.
Amesema kuwa mbolea hiyo imetolewa bure kwa wakulima wote nchini hivyo asijitokeza mtu katikati akaanza kuuza mbolea hiyo jambo ambalo litakuwa kinyume na matakwa ya programu hiyo.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema kuwa Lengo la mradi huo ni kukuza uzalishaji wa mahindi na mpunga ili kujihakikishia nchi inakuwa na chakula cha kutosha.
Amesema kuwa sekta ya kilimo ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi hivyo juhudi za kampuni ya Mbolea ya YARA zimekuja wakati muafaka wakati ambapo serikali inaendelea kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima nchini.
Waziri Hasunga ameongeza kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imeendelea kuweka msisitizo katika sekta ya kilimo ili malighafi za kutosha ziweze kupatikana kwa ajili ya viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya YARA Tanzania Winstone Odhiambo amesema kuwa pamoja na ugawaji huo wa mbolea lakini wakulima watapata elimu kutoka katika kampuni hiyo kuhusu mbinu za kisasa za kidijitali za kuongeza uzalishaji ili kuhakikisha nchi inazalisha chakula cha kutosha.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment